MCHEZAJI
wa Kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama, anaechezea Klabu ya Scotland,
Celtic, yuko mbioni kujiunga na Klabu za BPL, Barclays Premier League
baada ya Ofa kadhaa kumiminika za kumnunua.
BJORN
KUIPERS, Refa kutoka Holland, ndie atakaechezesha Fainali ya Mashindano
ya FIFA ya Kombe la Mabara itakayochezwa Jumapili Usiku Uwanja wa
Maracana huko Rio De Janeiro kati ya Wenyeji Brazil na Mabingwa wa Dunia
Spain.
KATIKA kuonesha kuwa bado uaminifu kwa wapenzi ni tatizo, juzikati
lilitokea fumanizi la aina yake baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika
kwa jina la Flaviana kumnasa mwanaume aliyedaiwa ni mumewe, aitwaye Aron
akifanya mapenzi na mwanamke mwingine.
Ni
aibu iliyoje! Mrembo mmoja, mkazi wa Kigogo, Dar es Salaam, aliyedaiwa
kuwa ni mchumba wa mtu ambaye jina lake halikupatikana, alikatikiwa
mshipa wa aibu na kuvua nguo katikati ya sherehe ya ‘birthday’ ya mtoto
PILIKAPILIKA
za Uhamisho wa Wachezaji zinaendelea na Klabu iliyopanda Daraja Msimu
huu, Hull City, imemsaini Mchezaji wa Kimataifa wa Egypt, Ahmed
Elmohamady,
FIFA
leo imetangaza Majina ya Wachezaji 6 watakaowania Tuzo ya Mchezaji Bora
wa Kombe la Mabara linalochezwa huko Nchini Brazil ambapo Mshindi wake
atatunukiwa Mpira wa Dhahabu wa Adidas.
MENEJA
MPYA wa Manchester United, David Moyes, anaanza kazi yake rasmi
Jumatatu ijayo na zipo taarifa kuwa Wiki hiyo hiyo atakamilisha Uhamisho
wa Thiago Alcantara kutoka Barcelona na Leighton Baines kutoka Everton.
Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika
Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio
nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita.
LEO
USIKU, Nusu Fainali ya pili ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara
inachezwa huko Estadio Castelao, Mjini Fortaleza Nchini Brazil kati ya
Mabingwa wa Dunia Spain na Italy kutafuta mpinzani wa Brazil ambao jana
walitinga Fainali baada ya kuifunga Uruguay Bao 2-1.
RVP, akihojiwa na Jarida la
Klabu yake Manchester United liitwalo ‘INSIDE UNITED’, aliongelea Msimu
wake wa kwanza na Klabu hiyo, ule wa 2012/13, na kutaja Matukio 20
yaliyomgusa.
KONA ya Dakika ya 86 ya Neymar ilimkuta Kiungo Paulinho aliejitwika
kichwani na kuipa Brazil Bao la pili na la ushindi na kutinga Fainali
ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara walipoifunga Uruguay Bao 2-1
katika Mechi ya Nusu Fainali iliyochezwa Estadio Mineirao, Mjini Belo
Horizonte, Nchini Brazil.
Uongozi
wa klabu ya Simba kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia
Hans Pope umetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango wao namba moja na mkongwe wa timu
hiyo Juma Kaseja.
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa
timu za Cosmopolitan na Taifa Stars, Mathias Kissa (84) kilichotokea
leo alfajiri (Juni 24 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) jijini Dar es Salaam.
KUNDI
B la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayochezwa huko Nchini
Brazil leo walicheza Mechi zao za mwisho na Mabingwa wa Dunia Spain
kuichapa Nigeria Bao 3-0 na Uruguay kuibamiza Tahiti Bao 8-0.
KOCHA
MPYA wa Bayern Munich, Mabingwa wa Ulaya na Germany, Pep Guardiola,
sasa anaanza rasmi kibarua chake kwa kuzungumza na Wanahabari hapo kesho
Jumatatu.
TONY
ADAMS, Nahodha wa zamani wa Arsenal, ameipasulia Klabu yake hiyo ya
zamani kwa kuwaambia wao bado sana kufikia hatua ya kutwaa Ubingwa na
badala yake wajitahidi kutwaa angalau FA CUP au Kombe la Ligi Vikombe
ambavyo pia amedai bado ni vigumu kwao.
LEO
huko Arena Fonte Nova, Mjini Salvador, Wenyeji Brazil wanapambana na
Italy katika Mechi ya mwisho ya Kundi A la Mashindano ya FIFA ya Kombe
la Mabara huku Timu zote zikiwa tayari zimeshatinga Nusu Fainali.