Sunday, June 23, 2013

KOMBE LA MABARA: SPAIN, URUGUAY ZIPO NUSU FAINALI, NIGERIA MAMBO YAGONGA MWAMBA NA TAHITI YAWA TISHIO


FIFA_CONFEDERATION_CUP_BRAZIL_2013KUNDI B la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayochezwa huko Nchini Brazil leo walicheza Mechi zao za mwisho na Mabingwa wa Dunia Spain kuichapa Nigeria Bao 3-0 na Uruguay kuibamiza Tahiti Bao 8-0.
Matokeo hayo yamezifanya Spain na Uruguay kuingia Nusu Fainali ambako Spain itacheza na Italy na Uruguay kuwavaa Wenyeji wa Mashindano Brazil.
NIGERIA 0 SPAIN 3
Bao za Jordi Alba, mbili, na Fernando Torres zimewapa Spain ushindi wa Bao 3-0 walipocheza na Nigeria na hivyo kutinga Nusu Fainali kama Vinara wa Kundi B ambapo watacheza Nusu Fainali na Timu ya Pili Kundi A ambayo ni Italy.
VIKOSI:
NIGERIA: Enyeama, Oboabona, Echiejile, Ambrose, Omeruo, Mikel, Ogude, Mba, Musa, Ideye, Akpala
Akiba: Ejide, Ogu, Egwueke, Mohammed, Kwambe, Ujah, Babatunde, Onazi, Eze, Oduamadi, Benjamin, Agbim.
SPAIN: Valdes, Arbeloa, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Pedro, Fabregas, Soldado
Akiba: Casillas, Albiol, Javi Martinez, Azpilicueta, Villa, Torres, Mata, Monreal, Cazorla, Silva, Jesus Navas, Reina.
REFA: Joel Aguilar (Slovakia)
URUGUAY 8 TAHITI 0
Uruguay wamefuzu kuingia Nusu Fainali baada ya kuifunga Tahiti Bao 8-0 na sasa watakutana na Wenyeji Brazil.
MAGOLI:
URUGUAY 8
- Abel Mathias Hernandez Dakika ya 2, 24, 45 & 67 [Penati]
-Diego Perez 27
-Nicolas Rodiero 62
-Luis Suarez 82 & 88
TAHITI 0
Licha ya ushindi huu, Uruguay hawakuacha ili asili yao ya utukutu baada ya Mchezaji wao Andres Scotti Ponce de Leon kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu mara baada ya kukosa kufunga Penati baada ya kupewa Kadi za Njano mbili.
Hata Tahiti walimaliza Mtu 10 baada ya Teheivarii Wagemann kupewa Kadi za Njano mbili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
VIKOSI:
URUGUAY: Silva, Aguirregaray, Scotti, Coates, Gargano, Pereira, Eguren, Lodeiro, Perez, Ramirez, Hernandez
Akiba: Muslera, Lugano, Godin, Rodriguez, Suarez, Forlan, Maxi Pereira, Arevalo Rios, Gonzalez, Cavani, Caceres, Castillo.
TAHITI: Meriel, Simon, Vallar, Ludivion, Caroine, Lorenzo Tehau, Aitamai, Jonathan Tehau, Hnanyine, Vahirua, Chong Hue
Akiba: Roche, Alvin Tehau, Wagemann, Bourebare, Faatiarau, Teaonui Tehau, Atani, Lemaire, Aroita, Tihoni, Vero, Samin.
REFA: Pedro Proenca (Portugal)
RATIBA:
NUSU FAINALI
Jumanne Juni 26
[Belo Horizonte]
[SAA 4 USIKU]
Brazil v Uruguay
Jumatano Juni 27
[Fortaleza]
[SAA 4 USIKU]
Spain v Italy
MSHINDI WA TATU
Jumapili Juni 30
[Salvador]
[SAA 1 USIKU]
FAINALI
Jumapili Juni 30
[Rio De Janeiro]

0 comments:

Post a Comment