Wednesday, June 26, 2013

RONALDO ATAKA KURUDI NYUMBANI AZUNGUMUZA NA WAKURGENZI WA MAN U,STEVEN GERRARD AKALIBISHWA UPYA

RONALDO_na_TUZO
MAN_UNITED-2013
MABINGWA Manchester United wamethibitisha kuondoka kwa Kocha wa Timu ya kwanza Rene Meulensteen wakati huko Spain zimeibuka stori kuwa Supastaa Cristiano Ronaldo atakutana na Maafisa wa Old Trafford Wiki ijayo kuzungumzio ujio wake kwa mara ya pili wakati huko Anfield kuna habari njema ya kupona kwa Nahodha na nguzo yao Steven Gerrard baada kufanyiwa operesheni.
KOCHA MEULENSTEEN
KLABU ya Manchester United leo imethibitisha kuwa Kocha waoMAN_UNITED-RENE wa Timu ya Kwanza, Rene Meulensteen, anaondoka Klabu hiyo akifuata nyayo za Makocha wenzake Mike Phelan na Eric Steele ambao walitangaza kuondoka mara tu baada ya Meneja Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu na David Moyes kuteuliwa Meneja mpya.
Inaaminika Rene Meulensteen amepata Ofa ya kwenda huko Urusi kuwa na Klabu ya Anzhi Makhachkala.
Baada ya kuthibitishwa kuondoka kwake, Meulensteen alitamka: “Napenda kumshukuru Sir Alex Ferguson, Wamiliki, Wafanyakazi wenzangu, Wachezaji na Mashabiki ambao waliufanya muda wangu hapa Manchester United uwe spesheli na ambao siwezi kuusahau! Namtakia kila Mtu hapa kwenye Klabu hii bora kila la heri!”
Meulensteen alijiunga na Man United Mwaka 2002 akitokea Al Sadd ya Qatar na kuondoka kwa muda mfupi Mwaka 2006 kwenda Brondby ya Denmark na kurudi baada ya Miezi 6 akiwa kama Kocha wa Timu ya Kwanza.
CRISTIANO RONALDO
RIPOTI toka huko Spain, kama zilivyochapishwa na Magazeti, zinadai kuwa Cristiano Ronaldo Wiki ijayo atafanya mazungumzo na Klabu ya Manchester United kuangalia uwezekano wa yeye kurudi tena Klabuni hapo ambako aliondoka Mwaka 2009 na kujiunga na Real Madrid.
Klabu ya Manchester United imekataa kuzungumza lolote kuhusu habari hizo.
Huku wakiwa na Meneja mpya, David Moyes, na kukiwa na uvumi mzito wa kuondoka kwa Straika wao, Wayne Rooney, hali ya baadae ya hapo Old Trafford bado haijulikani ingawa inaaminika Wiki ijayo itatoa fununu kubwa mara baada ya Julai Mosi Moyes kuanza wadhifa wake rasmi.
Mbali ya Man United, Ronaldo pia anaripotiwa kuwindwa na PSG na Chelsea huku Real yenyewe ikikaza uzi Staa huyo haondoki na mwenyewe kubaki ‘bubu!’
STEVEN GERRARDGERRARD
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard, ambae alifanyiwa upasuaji kutibu Bega lake, amesema anaendelea vizuri na anatarajia kuanza Mazoezi na wenzake watakapoanza kujitayarisha kwa ajili ya Msimu mpya.
Gerrard, Miaka 32, Msimu uliopita uliomalizika Mwezi Mei, alizikosa Mechi mbili za Liverpool za mwisho za Ligi dhidi ya Fulham na Queens Park Rangers baada ya Bega lake kuwa kwenye hali mbaya.
Gerrard Mwaka 2012-13
MECHI ZA LIGI: 36
MAGOLI: 9
Kwa zaidi ya Miezi mitatu, Gerrard alikuwa akicheza huku akisumbuliwa na Bega lakini baadae hali ikawa mbaya na ikabidi afanyiwe operesheni haraka.
Habari hii ya kupona kwa Gerrard pia ni habari njema kwa England, ambae yeye ni Nahodha, ambao hapo Septemba 6 na 10 wana Mechi muhimu mno dhidi ya Moldova na Ukraine za kuwania kwenda Brazil Mwaka 2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia.Www.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment