Friday, June 28, 2013

ALCANTARA AMFANYA MOYES KUKOSA AMANI

ALCANTARA_n_BAINES


MENEJA MPYA wa Manchester United, David Moyes, anaanza kazi yake rasmi Jumatatu ijayo na zipo taarifa kuwa Wiki hiyo hiyo atakamilisha Uhamisho wa Thiago Alcantara kutoka Barcelona na Leighton Baines kutoka Everton.
Thiago Alcantara
Gazeti la kuaminika huko Nchini Spain, AS, limedai Manchester United itakamilisha Wiki ijayo kumsaini Kiungo Chipukizi wa Spain Thiago Alcantara kutoka Barcelona.
Mapema Wiki hii ripoti kutoka Spain zilidai Kiungo huyo alishafikia makubaliano na Man United kuhusu maslahi yake binafsi na Uhamisho utakamilika pale Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa rasmi Julai 1.
David Moyes anaanza kazi yake rasmi Siku hiyo hiyo Julai 1 na inaaminika anataka kukamilisha usajili huu haraka ili ashughulikie maeneo mengine kwenye Kikosi chake.
Lakini, habari toka ndani ya Barcelona zinadai kuna ushawishi mkubwa unafanywa ili Mchezaji huyo abakie huko Nou Camp.
Staa wa Barca, Gerard Pique, alikaririwa akisema: “Upo uwezekano ataondoka lakini lazima tumshawishi sehemu bora kwake ni kubakia hapa!”
Leighton Baines
Baada ya Ofa yao ya Pauni Milioni 12 kukataliwa na Everton, inasadikiwa Man United wataongeza Dau lao la kufikia Pauni Milioni 16 ili kumnunua Fulbeki wa kushoto Leighton Baines mwenye umri wa Miaka 28.
Uamuzi wa kumnunua Baines sasa unaleta wasiwasi kuhusu hatima ya Beki Patrice Evra, Miaka 32, ambae amedumu Old Trafford Miaka 7 na nusu.
Zipo taarifa za Evra kuhusishwa na kurudi kwao France kujiunga na Monaco au Paris Saint-Germain.
Baines alinunuliwa na Moyes kutoka Wigan Mwaka 2007 na hata Msimu uliompita Man United, wakiwa chini ya Meneja Sir Alex Ferguson, walitaka kumnunua Baines lakini Everton, chini ya Meneja wao David Moyes, iliweka Dau la Pauni Milioni 18 na Man United wakaikataa Dili hiyo.
Hivi sasa, Baines amebakisha Mkataba wa Miaka miwili na Everton na inaelekea Everton watashawishika kumuuza Kwa Pauni Milioni 16.
posted by www,Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment