Tuesday, December 3, 2013

JE WAJUA? KABILA GANI ZURI NA LENYE SIFA ZA KUOA/KUOLEWA?



Sijajua kwa nini nimeamua kuandika mada hii, ila nimejikuta tu nikiandika. Lakini nina sababu ambayo nadhani inatosha kukushawishi hata wewe tukajiuliza kwa pamoja.

Nimewahi kukutana sana na swali hili na baadhi ya watu wakilizungumzia kwa namna ya kukebehi, kukejeli, kusifu na kuponda baadhi ya makabila linapofika suala la uhusiano wa kimapenzi au maisha ya ndoa.
“Umeoa Mmachame?, umekwisha, hao watu wabaya sana aisee,…
NINAWASALIMU kwa jina la Bwana, hasa wakati huu mamilioni ya Wakristo kote duniani wakijiweka sawa kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo wa Nazareti, zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Sijajua kwa nini nimeamua kuandika mada hii, ila nimejikuta tu nikiandika. Lakini nina sababu ambayo nadhani inatosha kukushawishi hata wewe tukajiuliza kwa pamoja. Nimewahi kukutana sana na swali hili na baadhi ya watu wakilizungumzia kwa namna ya kukebehi, kukejeli, kusifu na kuponda baadhi ya makabila linapofika suala la uhusiano wa kimapenzi au maisha ya ndoa.
“Umeoa Mmachame?, umekwisha, hao watu wabaya sana aisee, hawaoni taabu kukuua warithi mali,” mtu mmoja alimshangaa mwenzake baada ya kumwambia kuwa mwanandoa mwenzake anatokea Kilimanjaro katika kabila hilo.
“Hao Wangoni bwana, wape hela watafikisha, lakini mwanamke hafiki aisee, wahuni sana hao,” mwanamke mmoja alimweleza shoga yake baada ya kumtaarifu kwamba anajiandaa kufunga ndoa na mchumba wake ambaye ni Mngoni kutoka Ruvuma.
“Unaishi na Mhaya? Duh, mtawezana kweli, maana hao jamaa wana majivuno?!” mwingine naye anamshangaa mwenzake.
Kwa jumla, katika jamii yetu, tunalo tatizo hili kwa kiwango kikubwa sana, tukibaguana kwa misingi ya dini, kabila, elimu na vitu vingine chungu mzima. Tumeacha kuzungumzia mapenzi kwa maana ya uhusiano, tumeangukia katika kujadili vitu ambavyo havihusiki kabisa.
Rafiki yangu mmoja aliniambia kwamba alilazimika kuomba ushauri kwa watu wazima na majirani, ili aweze kushusha presha ya mama yake ambaye alikataa katakata mpango wake wa kuoa mwanamke anayetokea katika kabila la Warangi, wanaotokea Kondoa mkoani Dodoma, kwa sababu ambazo hazikumtosheleza hata kidogo.
Aliniambia kuwa mama yake alimweleza kuwa wanawake wa kabila hilo ni watu wanaopenda sana kutumia ushirikina katika uhusiano au ndoa zao.
Nimesikia mazungumzo ya namna hii kwa miaka mingi, nimejaribu kuchunguza kwa kuulizauliza watu wa makabila tofauti walio katika uhusiano na hata kusoma baadhi ya tafiti, inaonyesha kuwa hakuna ukweli wowote katika mapenzi yanayohusiana na tabia za kabila.
Hakuna uhusiano wowote kwa mfano, majivuno ya Mhaya na jinsi atakavyoishi kimapenzi na mwanamke ambaye wako kabila tofauti. Ni kweli, kwa nje, inaonekana kama hawa jamaa ni watu wa majivuni, lakini niwe mkweli kuwa ninao marafiki wengi Wahaya, lakini hawana majivuno hata kidogo.
Umalaya, ujivuni, ushirikina, uroho wa mali na vitu vingine, ni tabia binafsi ya mtu. Kulisingizia kabila ni kutotenda haki kwa sababu kwa mfano, wakati tukiambiwa kuwa wanaume wa Kingoni ni watu wa wanawake sana, upo ushahidi wa wazi kwamba Ruvuma si miongoni mwa mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya gonjwa hatari la Ukimwi!
Mtu anapaswa kufanya uamuzi wa kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na mtu kwa kufuata hisia zake na jinsi mwenyewe anavyomchukulia mwenza wake. Kuchagua kabila kama ndicho kigezo cha kuishi katika uhusiano ni ubaguzi, kitu ambacho ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Wengi wameshangazwa na kuimarika kwa uhusiano wao ambao awali ulitiliwa mashaka na watu wengi. Wazee wetu vijijini wangependa tuoe au kuolewa na watu wa kabila letu, lakini katika dunia inayojikusanya kwa kiwango kikubwa na kuwa kijiji, fikra hizi zimepitwa na wakati.
Kitu cha msingi ni kuangalia na kuzifanyia kazi sifa unazozitaka kutoka kwa mpenzi wako. Kama ana upungufu, mchukulie yeye kama yeye na siyo kabila, dini au elimu yake. Mapenzi ni sanaa, ambayo ndani yake haina ukabila, usomi wala imani!
Poste by http://thesuperonenews.blogspot.com/

7 comments:

  1. Nieisoma mada yako vizuri sana. Japo nimeipenda lakini sikuridhika na maoni yako. Umejitahidi kukwepa lawama ili usilaumiwe na makabila husika. Ukweli ni kuwa maoni uliyoyasikia toka kwa watu mbalimbali juu ya tabia za makabila ndiyo ukweli ulivyo. Kwa bahati mbaya hujafanya utafiti juu ya jambo hilo. Mimi kwa kiasi nimejaribu na maoni niliyoyapata kwa bahati nzuri yalitolewa na watu wa makabila husika ambao hawakutaka kujipendelea. Ni ukweli usiopingika kuwa pamoja na tabia kuwa ya mtu binafsi, zipo tabia ambazo zinaambatana na ukabila. Na hii inatokana na mila na malezi ya makabila hayo. Uchoyo kwa mpare siyo jambo la siri. ufundi wa mapenzi kwa mtoto wa kitanga si ajabu. Majivuno kwa mhaya sio siri. Hasira kwa mhehe si ajabu. Ulimbukeni kwa mgogo ni kitu cha kawaida. Juju kwa mrangi na mfipa ni kawaida. Ukarimu kwa mnyamwezi hauna ubishi. Michepuko kwa mngoni ni kama jadi. Ukatili kwa mchaga hauna mjadala. Umbeya kwa mzaramo ni sifa. Huruma kwa wayao haina mipaka. Mikato kwa wanyakyuka haina maswali ni maji mara moja. Huwezi kuyajua haya mpaka utembee sana. Lakini katika hali ya kawaida ukiwaeleza wenyewe lazima watakunja ngumi; ila ukweli unabaki palepale kuwa makabila hayafanani na watu ni wa makabila. Huwezi kusema mzungu na mswahili ni sawasawa tunapokuja kwenye tabia. Ila wazungu wanaweza kufanana na waswasili nao kufanana. Imetolewa na http://kivulinikwetu. blogspot.com

    ReplyDelete
  2. mimi ni mpare lakini sio mchoyo hata kdogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bado mnakwepa ukweli moare Ni mchoyo na bahili yote yake min nafanya kazi Same Hawa watu Ni hatar hawana ukalimu kama kama was Iringa kama Ni kabila lako sorry Ila kwenye ukweli tuseme ili tupone

      Delete
  3. ameshindwa kutofautisha kati ya uchoyo na ubahili wapare wao ni wabahili sio wachoyo

    ReplyDelete
  4. Chunguza kabila na familia ya mkena mama ya make atokeako wakoje ndipo uamua kuchukua uamzi was kuoa

    ReplyDelete