Wednesday, June 26, 2013

ROBIN VAN PERS : AAMUA KUFUNGUKA MAN UNITED! LITAKALO KUWA NA LIWE!!!!

RVP-BUTI_LA_DHAHABU 
RVP, akihojiwa na Jarida la Klabu yake Manchester United liitwalo ‘INSIDE UNITED’, aliongelea Msimu wake wa kwanza na Klabu hiyo, ule wa 2012/13, na kutaja Matukio 20 yaliyomgusa.
PATA MATUKIO HAYO:
1. KUTUA OLD TRAFFORD: “Nakumbuka nilikuwa na furaha sana! Changamoto hii mpya ilinifanya nipande joto!”
2. MAZOEZI YA KWANZA: “Nilichelewa kuanza mazoezi kwani nilikuwa namalizia kupima afya. Nilikuwa na hamu sana kuanza Mazoezi! ”
3. GEMU YA KWANZA (EVERTON 1 UNITED 0): “Niliingizwa zikiwa zimabaki Dakika 20 kule Everton! Ingawa tulifungwa lakini ilikuwa Siku kubwa! Nilisikia fahari kubwa kucheza Mechi yangu ya kwanza!”
4. MECHI YA KWANZA OLD TRAFFORD (UNITED 3 FULHAM 2) “Ulikuwa mwanzo mzuri na nilifunga baada ya Dakika 10. Ni Siku njema! Nilicheza Dakika 90 lakini baada ya Dakika 60 nilijikokota!”
5. HETITRIKI (Southampton 2 United 3): “Ilikuwa Gemu ya kiwetu na hatukukata tamaa. Niliomba radhi kwa wenzangu kwa kukosa Penati!”
6. BAO LA USHINDI ANFIELD (Liverpool 1 United 2): “Safari hii nilihakikisha nafunga Penati yangu. Nilijisikia safi kufunga Bao la Ushindi dhidi ya Liverpool.”
7. BAO 2 ULAYA (Cluj 1 United 2) “Ilikuwa pasi murua toka kwa Wazza kwa Bao langu la pili.”
8. DARAJANI (CHELSEA 2 UNITED 2): “Napenda kucheza dhidi ya Chelsea na nimefunga Goli FERGIE_n_RVPzangu zote dhidi yao Stamford Bridge. Ni sehemu murua kucheza na kushinda.”FERGIE_N_RVP_CELEBRATING
9. KUWANYUKA ARSENAL (United 2 Arsenal 1): “Ni Siku ya ajabu. Sijawahi kucheza dhidi ya Timu yangu ya zamani na kufunga Bao. Lakini hii ni kazi yetu.”
10. DABI (Man City 2 United 3) “Rooney na mimi tulijadiliana kuhusu frikiki! Shuti au krosi? Shuti lagu lilitinga baada ya kumparaza Beki!”
11. UPTON PARK (West Ham 2 United 2): “Goli mwishoni toka krosi ya Giggs! Sikusita, niliunganisha na kupata sare na Mechi ya marudio!”
12. SARE (Spurs 1 United 1): “Kulikuwa na barafu na baridi! Nilifunga! Lakini ni matokeo ndio nayakumbuka zaidi baada wao kusawazisha mwishoni!”
RVP_FRIKIKI213. TULIWAPIGA (UNITED 2 EVERTON 0): “Nilifunga lakini nadhani ilikuwa bahati. Ni ushindi mzuri ukikumbuka Sare ya 4-4 Msimu uliopita!”
14. SANTIAGO BERNABEU (Real Madrid 1 United 1): “Ni Uwanja wa Kihistoria Duniani! Ni mara ya kwanza kucheza pale! Tulikuwa na nafasi ya kushinda!”
15. NGUMU KUAMINI (UNITED 1 REAL 2): “Ni Kadi Nyekundu asiyostahili Nani! Ni pigo na ilibadilisha gemu!”
16. KUIFUNGA STOKE (STOKE 0 UNITED 2): “Wenzangu walinicheka nilipofunga Goli na kushangilia vile na kumbeba Sir Alex! Ni furaha tupu kuwa na Sir Alex!”
17. KUISHANGILIA SPURS: “Niliwashangilia Spurs walipocheza na City. Unaweza kuamini hilo? Mchezaji wa zamani wa Arsenal akitaka Spurs ishinde? Tulijua Ubingwa umebaki Gemu moja tu!”
18. LILE GOLI (UNITED 3 VILLA 0): “Kilikuwa kitu cha papo kwa papo! Nilitazama juu na kuona mpira uko juu na nilijua ni safi kuutuliza! Kila kitu kilienda sawa! Ni pasi murua ya Wazza!”
19. KOMBE LA UBINGWA: “ Hii ni kwa ajili ya Mashabiki, Wachezaji na Wafanyakazi wa Klabu! Kitu ambacho kimenifurahisha ni kwamba Watu wengi walifurahi! Watoto, Wanawake, Wanaume-wote walikuwa na furaha kubwa!”
20. USIKU WA TUZO: “Kutwaa Taji la Mchezaji Bora wa Mwaka ni kitu kizuri sana. Kushirikiana na wenzangu ni kitu muhimu sana! Ni furaha kubwa kufanya nao kazi!

0 comments:

Post a Comment