KONA ya Dakika ya 86 ya Neymar ilimkuta Kiungo Paulinho aliejitwika
kichwani na kuipa Brazil Bao la pili na la ushindi na kutinga Fainali
ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara walipoifunga Uruguay Bao 2-1
katika Mechi ya Nusu Fainali iliyochezwa Estadio Mineirao, Mjini Belo
Horizonte, Nchini Brazil.
MAGOLI:
BRAZIL
-Fred Dakika ya 42
-Paulinho 86
URUGUAY
-Cavani Dakika ya 48
Lakini ilikuwa kazi njema ya Neymar
alieshusha pasi ndefu ya Luis Gustavo kifuani akiwa ndani ya boksi na
kugonga mpira ulioguswa na Kipa Muslera na kumkuta Fred aliemalizia
vizuri na kuweka Bao la kwanza kwa Brazil.
Uwanja mzima ulishangilia sana Bao hili hasa kwa vile Fred ni ‘Mtoto wa Nyumbani’ hapo Estadio Mineirao.
Uruguay walisawazisha Kipindi cha Pili
Dakika ya 48 baada ya makosa ya Mabeki wa Brazil Thiago Silva aliemuuza
Marcelo na Edinson Cavani kuunasa mpira na kufunga.
Wenyeji Brazil hawakuvunjika moyo na
waliendelea kusakata kabumbu na Uruguay kusimama imara hadi Dakika ya 86
ushindi ulipopatikana.
Kwenye Fainali Jumapili Brazil watacheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine itakayocheza Alhamisi Usiku kati ya Spain na Italy.
VIKOSI:
BRAZIL: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar, Gustavo, Paulinho, Fred, Hulk, Neymar
Akiba: Jefferson, Fernando, Lucas Moura, Hernanes, Dante, Filipe Luis, Jean, Rever, Bernard, Jo, Jadson, Cavalieri.
URUGUAY: Muslera, Lugano, Godin, Caceres, Maxi Pereira, Rodriguez, Arevalo Rios, Gonzalez, Forlan, Suarez, Cavani
Akiba: Castillo, Coates, Gargano, Pereira, Eguren, Hernandez, Aguirregaray, Lodeiro, Perez, Ramirez, Silva.
Refa: Enrique Osses (Chile)
RATIBA/MATIBA:
NUSU FAINALI
Brazil 2 Uruguay 1
Alhamisi Juni 27
[Fortaleza]
[SAA 4 USIKU]
Spain v Italy
MSHINDI WA TATU
Jumapili Juni 30
[Salvador]
[SAA 1 USIKU]
FAINALI
Jumapili Juni 30
[Rio De Janeiro]
[SAA 7 USIKU]
Brazil v Spain/Italy Posted by WWW.Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment