Saturday, June 29, 2013

KOMBE LA MABRA Andres Iniesta Spain pamoja na -Neymar Brazil ndani ya kuwania tuzo YA dhahabu

ADIDAS_GOLDEN_BALLFIFA leo imetangaza Majina ya Wachezaji 6 watakaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Mabara linalochezwa huko Nchini Brazil ambapo Mshindi wake atatunukiwa Mpira wa Dhahabu wa Adidas.
Wachezaji wote hao 6 wanatoka Timu za Brazil, Italy, Spain na Uruguay ambazo ndizo zilifika Nusu Fainali na Majina yao kuteuliwa na FIFA Technical Study Group (TSG) lakini Mshindi atapatikana kwa Kura za Wanahabari maalum walioruhusiwa kwenye Mashindano hayo.
Mshindi wa Tuzo hii atatangazwa mara baada ya Fainali kati ya Brazil na Spain kumalizika Jumapili Usiku.
Mshindi wa Pili wa Tuzo hii atapewa Mpira wa Fedha wa Adidas na wa tatu kupewa Mpira wa Adidas wa Shaba.
WAGOMBEA WA TUZO YA ADIDAS MPIRA WA DHAHABU NI:
-Andres Iniesta (Spain
-Neymar (Brazil
-Paulinho (Brazil)
-Andrea Pirlo (Italy)
-Sergio Ramos (Spain)
-Luiz Suarez (Uruguay)
WASHINDI WALIOPITA WA TUZO HII:
-1997 - Denilson (Brazil)
-1999 - Ronaldinho (Brazil)
-2001 - Robert Pires (France)
-2003 - Thierry Henry (France)
-2005 - Adriano (Brazil)

0 comments:

Post a Comment