Tuesday, June 11, 2013

KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014: MESS LEO HATIHATI KUCHEZA ECUADOR v ARGENTINA

ARGENTINA NJIA NYEUPE BRAZIL WAKISHINDA…..!!
LAKINI HUKO QUITO HAWAJASHINDA TANGU 2001……!!
CAICEDO, HATI HATI KUCHEZA!!
MESSI_IN_ARGENTINAVINARA wa Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil, Argentina wanasafiri kwenda kucheza Mjini Quito dhidi ya Ecuador na ushindi kwao utawafanya njia iwe nyeupe kwenda Brazil lakini hawajahi kushinda huko tangu Mwaka 2001.
Katika mara mbili zao walizocheza mwisho huko Quito, Argentina wamefungwa Mechi zote na sasa wanaivaa Ecuador ambayo imeshinda Mechi zao zote 6 za Mashindano haya ya Kombe la Dunia walizocheza Nyumbani na kufunga Bao 13 kati ya Jumla ya 16 walizofunga kwenye michuano hii.
Lakini pande zote zina hati hati ya kuwakosa Mastaa wao wakubwa ambao wana maumivu kwa Argentina kuwa na wasi wasi na Lionel Messi na Ecuador kumuuguza Felipe Caicedo.
Mbali ya Mechi hii ya Ecuador v Argentina hii Jumanne pia zipo Mechi nyingine 3 za Kanda hii kuwania kwenda Brazil.
Timu 4 za Juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka Kanda ya ASIA kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.
RATIBA
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Ijumaa Juni 7
Bolivia 1 Venezuela 1
Jumamosi Juni 8
Argentina 0 Colombia 0
Paraguay 1 Chile 2
Peru 1 Ecuador 0
Jumanne Juni 11
23:30 Colombia v Peru [1-0]
00:00 Ecuador v Argentina [0-4]
Jumatano Juni 12
01:00 Venezuela v Uruguay [1-1]
01:30 Chile v Bolivia [2-0]
Jumapili Septemba 8
01:00 Colombia v Ecuador [0-1]
01:00 Chile v Venezuela [2-0]
01:00 Paraguay v Bolivia [1-3]
01:00 Peru v Uruguay [2-4]
Jumanne Septemba 10
03:00 Bolivia v Ecuador [0-1]
03:00 Paraguay v Argentina [1-3]
0300  Venezuela v Peru[1-2]
03:00 Uruguay v Colombia [0-4]
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Argentina
11
7
4
1
24
8
16
25
2
Colombia
11
6
2
3
19
7
12
20
3
Ecuador
11
6
2
3
16
11
5
20
4
Chile
12
6
0
6
18
20
-2
18
5
Venezuela
12
4
4
4
10
13
-3
16
6
Peru
11
4
2
5
12
15
-3
14
6
Uruguay
11
3
4
4
17
21
-4
13
8
Bolivia
12
2
4
6
14
21
-7
10
9
Paraguay
12
2
2
8
9
23
-14
8
**FAHAMU: Timu 4 za Juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka Kanda ya ASIA kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.

0 comments:

Post a Comment