MSHAMBULIAJI
Samuel Eto's jana amerudia kushangilia kama kikongwe baada ya kuifungia
Cameroon bao la kuongoza ikitoka safe ya 2-2 na Ujerumani katika mchezo
wa kirafiki kujiandaa na Kombe la Dunia.
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 33 alimtoka beki Mats Hummels kuuwahi mpira
kabla ya kumtungua kioa wa Ujerumani, Roman Weidenfeller dakika ya 62.
Eto'o,
alishangilia kama hivyo awali katika klabu yake Chelsea baada ya
kufunga dhidi ya Manchester United katika Ligi Kuu ya England, kujibu
mapigo ya kocha wake, Mreno Jose Mourinho aliyehoji umri wake akidai ni
mkubwa kuliko miaka anayotaja. Bao lingine la Cameroon lilifungwa na
Choupo-Moting dakika ya 78, wakati mabao ya Ujerumani yalifungwa na
Muller dakika ya 66 na Schurrie dakika ya 71.
Kikosi
cha Ujerumani kilikuwa: Weidenfeller, Boateng, Mertesacker, Hummels,
Durm/Howedes, dk85, Khedira/Kramer, dk73, Kroos, Muller, Ozil/Podolski,
dk63, Reus, Gotze/Schurrle, dk58.
Cameroon:
Itandje, Djeugoue, Bedimo/Assou-Ekotto, dk58, N'Koulou, Song,
Mbia/N'Guemo, dk46, Enoh, Matip, Choupo-Moting, Moukandjo, Eto'o/Webo,
dk90.
La kwanza: Samuel Eto'o akifunga bao la kwanza la Cameroon katika safe ya 2-2 na Ujerumani jana
0 comments:
Post a Comment