Sunday, June 23, 2013

MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL TONY ADAMS AIAMBIA ARSENAL BADOSANA UBINGWA ,ATOA USHAURI

TONY_ADAMS_N_SOL_CAMPBELLTONY ADAMS, Nahodha wa zamani wa Arsenal, ameipasulia Klabu yake hiyo ya zamani kwa kuwaambia wao bado sana kufikia hatua ya kutwaa Ubingwa na badala yake wajitahidi kutwaa angalau FA CUP au Kombe la Ligi Vikombe ambavyo pia amedai bado ni vigumu kwao.

APINGA UTEUZI WA CHIPS!!ATOA OFA YA KUWEKWA KWENYE BODI ILI KUISAIDIA!  

AITAKA ARSENAL IANZE MKAKATI KUMSAKA MBADALA WA WENGER!

Vile vile, Tony Adams amesisitiza kuwa Klabu hiyo haijajitayarisha jinsi ya kumbadili Arsene Wenger ikiwa Meneja huyo ataamua kuondoka mwishoni mwa Msimu huu unaokuja wakati Mkataba wake utakapomalizika.
Adams amebatuka: “Umefika wakati wa Arsenal kutwaa Taji lolote hata kama ni kutwaa FA CUP au Kombe la Ligi. Lakini ukweli hilo silioni. Bado hawajakamilika kwa maeneo fulani kwenye Timu. Na Ubingwa uko mbali sana kwao!”
Vile vile, Tony Adams, mwenye Miaka 46, alitoboa: “Nilitoa ofa ya kujiunga na Bodi ili niwasaidie lakini sikujibiwa!”
Pia Adams alidai kustushwa kwake na uteuzi Sir Chips Keswick, mwenye Miaka 73, kuwa Mwenyekiti wa Arsenal, uteuzi ambao ulifanyika Wiki iliyopita.
Adams alisema: “Chips ni Mtu mwema lakini huu uteuzi wa Wamiliki Klabu si sahihi! Huyu ana Miaka 73! Kama wangetaka Mtu Bora na mbunifu wangenichagua mimi na si Chips!”
Wenger, ambae kwa Miaka minane sasa hajatwaa Kombe lolote, anadaiwa kuwa atarudi kwao France Mkataba wake ukimalizika Mwakani ili ajiunge na Paris Saint-Germain.
Akigusia hilo, Adams alitamka: “Huu ni wakati muafaka kuaanza kusaka Meneja mpya!”

0 comments:

Post a Comment