LEO
USIKU, Nusu Fainali ya pili ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara
inachezwa huko Estadio Castelao, Mjini Fortaleza Nchini Brazil kati ya
Mabingwa wa Dunia Spain na Italy kutafuta mpinzani wa Brazil ambao jana
walitinga Fainali baada ya kuifunga Uruguay Bao 2-1.
Nao Italy ndio wameathirika sana na
majeruhi baada ya Wachezaji wao wawili kurudishwa Nyumbani baada ya
kuumia na alitangulia Fulbeki Abate na Juzi kufuatia Straika Mario
Balotelli.
Pia, Kiungo Mkongwe Andrea Pirlo
aliikosa Mechi na Brazil Jumamosi iliyopita kwa kuwa na maumivu lakini
leo anatarajiwa kucheza pamoja na Montolivo ambae alikuwa kaumia.
Vile vile Kiungo Daniele De Rossi
anaweza kucheza Mechi hii baada ya kuikosa ile na Brazil baada ya kuwa
kwenye Kifungo cha Mechi moja.
Timu zote, Spain na Italy, hazina Mchezaji alie Kifungoni.
Tathmini ya Mechi
Spain wanatoka kwenye ushindi mnono
baada ya kuitwanga Nigeria 3-0 katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi B na
kumaliza hatua hiyo wakionyesha wana Difensi nzuri na Fowadi hatari
katika Mashindano haya.
Kitu kingine cha faida kwa Spain ni kuwa
Straika wao Fernando Torres ameonyesha yuko imara baada ya kufunga Bao
5, 4 dhidi ya Tahiti walipoibamiza 10-0 na moja dhidi ya Nigeria, na
hilo linatia moyo kuwa atamudu kucheza vyema ikiwa Soldado, ambae ndie
kawaida huanza Mechi, atashindwa kucheza.
Italy wanatoka kwenye kipigo cha Bao 4-2
toka kwa Brazil lakini walicheza Mechi hiyo bila nguzo zao imara kwenye
Kiungo kwa kuwakosa Pirlo na De Rossi.
Lakini pia wataingia kwenye Mechi bila
ya Straika wao Balotelli na hivyo watalazimika kumchezesha Gilardino au
El Shaarawy kama Straika pekee kwa mujibu wa Mfumo wao wa 3-4-2-1.
Uso kwa Uso
Tangu Mwaka 1924, Spain na Italy zimekutana mara 27 na kila Timu imeshinda mara 8 na Sare 1.
Mara za mwisho kukutana ni kwenye EURO
2012 ambako walikuwa Kundi moja na kutoka Sare Bao 1-1 na kisha kukutana
tena kwenye Fainali na Spain kushinda Bao 4-0 kwa Bao za Silva, Alba,
Torres na Mata.
VIKOSI VONATARAJIWA:
SPAIN [Mfumo: 4-3-3]:
Casillas
Arbeloa-Ramos-Piqué-Alba
Xavi-Busquets-Iniesta
Pedro-Torres-Silva
ITALY [Mfumo: 3-4-2-1]:
Buffon
Barzagli-Chiellini -Bonucci
Maggio-Pirlo-Rossi -Giaccherini
Candreva-Marchisio
Gilardino
REFA: Howard Webb [England]
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
Jumatano Juni 26
Brazil 2 Uruguay 1
Alhamisi Juni 27
[Fortaleza]
[SAA 4 USIKU]
Spain v Italy
MSHINDI WA TATU
Jumapili Juni 30
[Salvador]
[SAA 1 USIKU]
FAINALI
Jumapili Juni 30
[Rio De Janeiro]
[SAA 7 USIKU]
Brazil v Spain/Italy
0 comments:
Post a Comment