Monday, June 24, 2013

MMILIKI AC MILAN AHUKUMIWA JELA MIAKA 7!!

BUNGA_BUNGA

ALIEKUWA Waziri Mkuu wa Italy ambae pia ndie Mmiliki wa Klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi amehukumiwa Kifungo cha Miaka 7 jela.
Berlusconi, ambae pia ni Rais wa Heshima wa AC Milan, alipatikana na hatia hii leo Mahakamani kwa kosa la kulipia ili afanye ngono na Changudoa ambae alikuwa chini ya Umri halali.
Mbali ya Kifungo hicho, pia Mahakama imemzuia asishike wadhifa wowote wa Umma hadi Rufaa yake imalizike.
AC_MILAN_MONTOLIVOInadaiwa, Berlusconi, Mwaka 2010 wakati akiwa Waziri Mkuu, alifanya ngono na Karima El Mahroug aliekuwa na Miaka 17 na pia alitumia wadhifa wake wakati huo ili Binti huyo atolewe Jela wakati alipowekwa ndani akiwa na mashitaka ya wizi wa udokozi.
Jopo la Majaji watatu leo ndio limetoa Hukumu hiyo kwenye Kesi ambayo Karima El Mahroug na Kundi la Wanawake wengine wanadaiwa kuhudhiria Pati kadhaa Nyumbani kwa Berlusconi ambazo zilipata umaarufu na kubandikwa Jina "bunga-bunga" kama mwenyewe Berlusconi alivyodhihaki wakati akiponda tuhuma dhidi yake na kuzipachika jina hilo.
Karima El Mahroug nae amekanusha tuhuma za kutembea na Berlusconi.
Mara baada ya Hukumu hiyo, Wanasheria wa Mmiliki huyo wa Klabu ya AC Milan walisema watakata Rufaa.
Mwaka Jana, Berlusconi alihukumiwa Kifungo cha Miaka minne kwa tuhuma za kukwepa kulipa Kodi na hadi sasa Kifungo hicho bado hakijaanza kwa vile amekata Rufaa.
Hata hiki Kifungo cha Miaka 7 hakitaanza hadi Rufaa yake imalizwe kusikilizwa kitu ambacho kinaweza kuchukua Miaka kadhaa.
NI ‘BUNGA-BUNGA’ YAMPONZA!!posted by www.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment