Thursday, February 20, 2014

HATARI!!!: MTOTO WA RAIS ANASWA AKIPIMA 'NGOMA'


Mwandishi wetu alimshuhudia Amini akiwa katika kituo hicho kupima ugonjwa huo katika siku hiyo ambayo huadhimishwa kama Siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ ili kutaka kujua afya yake na kuwa tayari majibu yake yawekwe hadharani.
Hata hivyo, baada ya vipimo na kutakiwa kusubiri majibu, Amini alionekana kuwa mnyonge na mwenye mawazo mengi ingawaje aliweza kujifariji kwa kuangalia runinga iliyopo katika chumba cha kusubiria majibu.
Alipoitwa kwenda kupatiwa majibu yake alijikuta akijikwaa zaidi ya mara tatu na alipoingia chumba cha majibu, nusura adondoke baada ya kujikwaa tena katika kizingiti cha mlango wa kuingia kwa daktari.
Mara baada ya kupewa majibu yake, Amin alisema amechukua uamuzi wa kuijua afya yake siku hiyo kwa sababu vijana wengi huitumia kwa ajili ya kufanya ngono katika nyumba za kulala wageni.
“Nimeamua kupima Ukimwi leo kwa sababu vijana wengi wamepanga kukutana na mpenzi wao kwa lengo la kufanya ngono,” alisema Amini ambaye alionekana kuwa na furaha baada ya kupata majibu mazuri.

0 comments:

Post a Comment