Saturday, June 29, 2013

KOMBE LA MABARA: FAINALI YA KESHO REFA ATANGAZWA!!


REFA_Bjorn_Kuipers 



















BJORN KUIPERS, Refa kutoka Holland, ndie atakaechezesha Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara itakayochezwa Jumapili Usiku Uwanja wa Maracana huko Rio De Janeiro kati ya Wenyeji Brazil na Mabingwa wa Dunia Spain.

Hii ni Fainali ya pili kubwa Mwaka huu kwa Refa Kuipers, mwenye Miaka 40, [Pichani kushoto] kwani pia alichezesha Fainali ya UEFA EUROPA LIGI Mwezi Mei kati ya Chelsea na Benfica.
Katika Mechi ya utangulizi ya kusaka Mshindi wa Tatu wa Kombe laREFA_Djamel_HaimoudiMabara kati ya Italy na Uruguay Refa atakuwa ni kutoka Nchi ya Algeria Djamel Haimoud mwenye Miaka 42 [Pichani kulia].
Refa Haimoud ndie aliteuliwa Refa Bora Afrika Mwezi Desemba 2012 katika Tuzo za CAF.
Kwenye Mashindano haya ya Kombe la Mabara Haimoud alichezesha Mechi ya Kundi B Spain ilipoitwanga Haiti Bao 10-0.
KOMBE LA MABARA
Jumapili Juni 30
MSHINDI WA TATU
[Salvador]
[SAA 1 USIKU]
Uruguay v Italy
FAINALI
[Rio De Janeiro]
[SAA 7 USIKU]
Brazil v Spain

0 comments:

Post a Comment