Sunday, June 23, 2013

SPAIN, TORRES, NIGERIA NA TAHITI ZIMEJIWEKEA REKODI NYINGINE KWENYE KOMBE LA MABARA BRAZIL

Hizi zifuatazo ni takwimu zilizojitokeza kwenye michezo ya juzi ya FIFA Confederation Cup baina ya Spain vs Tahiti na Uruguay vs Nigeria.

 - Diego Lugano alimaliza ukame wa goli ambao umedumu kwa miezi 18 - mara ya mwisho kufunga ilikuwa kwenye kombe la Ufaransa akiwa na PSG mwezi January 2012.
 
 - Diego Forlan pia nae alimaliza ukame wa mabao, juzi alifunga bao kwa upande wa Uruguay kwa mara ya kwanza tangu alipofunga dhidi ya Venezuela tarehe 2 June 2012.


 - Kipigo walichopata Nigeria kutoka kwa Uruguay kinamaanisha kwamba wamepoteza rekodi yao ya kutowahi kufungwa kwenye michuano hii. Denmark sasa ndio inabaki kuwa timu pekee kutowahi kufungwa kwenye historia ya michuano hii. 



 - Ushindi wa mabao 10-0 wa Spain dhidi ya Tahiti ulikuwa ndio mkubwa kuliko wowote uliowahi kutokea kwenye historia ya michuano ya mabara - ukivunja rekodi ya ushindi wa Brazil 6-0 Australia mwaka 1997 na Brazil 8-2 Saudi Arabia mwaka 1999.

 - Pia ushindi wa Spain wa 10-0 ulifikia rekodi ya uwepo wa mabao mengi katika mechi moja (Brazil 8-2 Saudi Arabia mwaka 1999)


- Fernando Torres aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat tricks mara mbili katika kombe la mabara - mara ya kwanza alifunga hat trick kwenye mchezo dhidi ya New Zealand mwaka 2009. 


 - Torres ni mchezaji wa tatu kufunga mabao manne katika mechi moja - wa kwanza Marzouk Al Otaibi na wapili ni Cuauhtemoc Blanco


 - Tahiti wamefikia rekodi ya kuruhusu mabao mengi kwenye kombe la mabara - wamefungwa jumla ya mabao 16 - rekodi hii iliwekwa na Saudi Arabia Saudi Arabia mwaka 1999

0 comments:

Post a Comment