Saturday, June 29, 2013

CHELSEA: WAELEKEA KUZURI KWA CAVANI MCHEZAJI APELEKWA SEVILLA!

EDINSON_CAVANI 
PILIKAPILIKA za Uhamisho wa Wachezaji zinaendelea na Klabu iliyopanda Daraja Msimu huu, Hull City, imemsaini Mchezaji wa Kimataifa wa Egypt, Ahmed Elmohamady,
wakati Stoke City imemnunua Beki wa Holland Erik Pieters kutoka PSV Eindhoven na Chelsea imemtoa Mchezaji wao Marko Marin kwa Mkopo kwenda Klabu ya Spain Sevilla.
Chelsea yamtoa Marko Marin kwa Mkopo Sevilla
Kiungo wa Chelsea Marko Marin anahamishiwa kwa Mkopo huko Spain kwa Klabu ya Sevilla.
Marin, Mjerumani mwenye Miaka 24, alisainiwa Chelsea kutoka Werder Bremen kwa Dau la Pauni Milioni 7 Msimu uliopita lakini akakumbwa na majeruhi na kucheza Mechi 16 tu.
Hivi sasa Chelsea imemnunua Andre Schurrle kutoka Bayer Leverkusen na hatua hii, bila shaka, ndio imelazimisha kuondoka kwa Marin.
Hata hivyo, Uhamisho huu wa Marin haujakamilika na bado unasubiri kupitishwa kwa taratibu za Kisheria kwa mujibu wa tamko la Klabu ya Chelsea.
Ahmed Elmohamady: Hull City yamsaini Kiungo wa SunderlandELMOHAMADY
Hull City imemsaini Mchezaji wa Kimataifa wa Egypt Ahmed Elmohamady kwa Ada ya Uhamisho ambayo haikutajwa ila Inasadikiwa kuwa Pauni Milioni 2 na amepewa Mkataba wa Miaka mitatu.
Msimu uliopita, Elmohamady alichezea Hull City kwa Mkopo akitokea Sunderland na kufunga Bao 3 katika Mechi 41 na kuisaidia Timu hiyo kupanda Daraja kuingia BPL, Barclays Premier League.
Hii ni mara ya pili kwa Meneja wa Hull City Steve Bruce kumsaini Elmohamady kwani Mwaka 2010 wakati Steve Bruce alipokuwa Meneja wa Sunderland alimchukua Mchezaji huyo kutoka Klabu ya Egypt ENPPI kwa Mkopo ambao baadae ulifanywa Uhamisho wa kudumu.
Akiongea, Elmohamady alisema: “Meneja ndie alienileta Sunderland kutoka Egypt na nasikia raha kucheza chini yake!”
Stoke City yamnunua Mholanzi Erik Pieters
Stoke City imekamilisha Uhamisho wa Beki wa Holland Erik Pieters kutoka Klabu ya PSV Eindhoven.
Pieters, Miaka 24, amesaini Mkataba wa Miaka minne na Dau lake la Uhamisho ni Pauni Milioni 3.
Uhamisho huu ni wa kwanza kwa Meneja mpya wa Stoke City, Mark Hughes, alIechukua wadhifa huo kutoka kwa Tony Pulis Mwezi Mei.
MVUTANO WA CAVANI
Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesisitiza kuwa hawatashusha Dau la kumuuza Straika wao hatari Edinson Cavani anaesakwa na Klabu kubwa za Ulaya.
Iliripotiwa kuwa Cavani, mwenye Miaka 26, anaamini Dau la Euro Milioni 65 linalowekwa kwenye Uhamisho wake ni kubwa mno ingawa hilo ndio lipo kwenye Kipengele cha Mkataba wake kwamba lazima lilipwe ikiwa Uhamisho utafanywa kabla Mkaba wake kumalizika.
Cavani mwenyewe anataka kuzungumza na Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis ili kuondoa utata na yeye kuhama.
Inaaminika Klabu za Real Madrid, Chelsea na Manchester City ndio zinazomtaka ingawa chaguo lake mwenyewe ni Real.
Lakini De Laurentiis ametamka: “Hamna haja ya mazungumzo ya uso kwa uso na Cavani. Kipo Kipengele na upo wakati Klabu zitalazimika kuleta Fedha hizo mezani. Hapo hatuwezi kumzuia.”WWW.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment