Wednesday, January 15, 2014

Ngono; sifa mpya inayotawala vyuo

Baadhi ya wakufunzi vyuoni wamekuwa wakidai ngono kama njia ya kuwapa alama za ufaulu wanafunzi.Picha ya Maktaba

  • Hali ni mbaya katika sekta ya elimu hasa kutokana na baadhi ya walimu kupenda ngono kama njia mbadala ya mwanafunzi kufaulu, badala ya uwezo wake thabiti.
  • Baadhi ya wachambuzi wanashauri kuwepo kwa mkakati makini wenye lengo la kufahamu kwa kina kuhusiana na suala hili la ngono vyuoni, kwani linaonekana ni la kawaida katika baadhi ya shule na vyuo.Uwepo wa sheria kali ni suala la msingi ili kuinusuru sekta ya elimu ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi kwa jumla

Ni jambo la kusikitisha lakini ndiyo ukweli kwamba kuna baadhi ya wenye mamlaka katika shule wanatumia madaraka yao kujipatia ngono kutoka kwa wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi tayari wamenaswa, huku wengine wakiambukizwa virusi vya Ukimwi au kuwa nyumba ndogo; sababu kubwa ni umalaya wa baadhi ya walimu, huku kukiwa na hofu juu ya nini hatma ya hali hii.
Mbaya zaidi ni kwamba mwalimu akiomba uhusiano kwa msichana, akikataa, baadhi yao huwaharibia wanafunzi hao kwa maana ya kuwapa alama mbaya katika mitihani yao, hata kama walifanya vizuri.
Wapo ambao wanashawishiwa na walimu kuingia kwenye ngono, pia wapo wanafunzi wanawashawishi walimu kuanzisha uhusiano nao ili kufanya masomo yawe mepesi.
Uhalisia wenyewe              
Ngono inapandisha alama za kufaulu vyuoni, inamfanya aliye na uwezo mdogo kuwa kinara darasani.
Imefika hatua baadhi ya wanachuo wanajipanga wakati wa mitihani yao, wanamtoa mmoja kafara kwa ajili ya wengine, anashawishiwa akajipendekeze, agawe penzi kwa mwalimu ikibidi ilimradi tu mambo yawe mepesi kwenye mtihani. Staili hii sasa inaitwa ‘kuzima moto’.
Mchezo huu umekuwa maarufu, si kwenye vyuo vingi. Linapotamkwa neno rushwa mara nyingi baadhi ya watu wanayaelekeza mawazo yao kwenye sehemu zinazotoa huduma muhimu kama vile mahakama, hospitali, polisi kutokana na sababu kuwa ni rahisi kuonekana.
Kupenyeza kwa kasi rushwa kwenye sekta ya elimu kunaweza kuelezwa kuwa kunachochea kwa kasi kushuka kwa elimu miongoni mwa wanajamii nchini. Kushuka huko kunaanzia ngazi za chini na katika kwenda ngazi za juu.
Hali hiyo inatia shaka ya kuwepo kwa wataalamu wasio na uwezo. Haya mambo ndiyo yanafanya kuwepo kudharauliwa kwa wasomi wengi siku hivi, na hata maisha ya baadhi ya wasomi yanadhihitisha hilo kwamba wengine elimu haiendani na uhalisia wao.
Lakini ni mara chache sana watuhumiwa wa kutoa au kupokea rushwa hiyo wamekuwa wanakamatwa kwa kuwa sehemu kubwa ya utoaji na upokeaji hufanyika kwa faragha
posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment