Saturday, June 29, 2013

MME WA MTU AFUMANIWA MENGI YAWEKWA WAZI

Mke akiwa amepigwa butwaa
 KATIKA kuonesha kuwa bado uaminifu kwa wapenzi ni tatizo, juzikati lilitokea fumanizi la aina yake baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Flaviana kumnasa mwanaume aliyedaiwa ni mumewe, aitwaye Aron akifanya mapenzi na mwanamke mwingine.
Tukio hilo lililowashangaza wengi lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika gesti moja iliyopo Sinza jijini Dar. Awali Flaviana na bwana wake huyo walichukua chumba baada…
Stori:Issa Mnally na Richard Bukos
KATIKA kuonesha kuwa bado uaminifu kwa wapenzi ni tatizo, juzikati lilitokea fumanizi la aina yake baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Flaviana kumnasa mwanaume aliyedaiwa ni mumewe, aitwaye Aron akifanya mapenzi na mwanamke mwingine.
Mke akiwa amepigwa butwaa
Tukio hilo lililowashangaza wengi lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika gesti moja iliyopo Sinza jijini Dar. Awali Flaviana na bwana wake huyo walichukua chumba baada ya kushindwa kurudi nyumbani kutokana na kuzidiwa na kilevi.
Kitanda kikiwa vululu
Ilikuwaje fumanizi likatokea?
Ilielezwa kuwa wakati wawili hao wakiingia kwenye chumba cha gesti hiyo, Flaviana alikuwa bwii hivyo ‘kuzima’ kwenye kochi na kushindwa kufanya chochote.
Akiangalia Suruali ya mumewe
“Wakati Aron akiwa chumbani pale, alifika shosti wa Flaviana aitwaye Dina na kwa kuwa Flaviana alikuwa hajitambui, wawili hao walianza kupeana malavidavi.
“Flaviana akiwa amelala alikuwa kama vile anasikia watu wakishughulika lakini alishindwa kufanya chochote kutokana na kuzidiwa na pombe.
“Wale wakaendelea kubanjuka. Ilipofika saa 12 asubuhi Flaviana akapata nguvu na kuamka kwenda kujisaidia, aliporudi akabaini shosti wake amemsaliti na ndipo alipoanzisha timbwili,” alidai mtoa habari wetu.
Flaviana apigia simu mapaparazi
Wakati timbwili hilo likiendelea chumbani hapo, Flaviana alipata mwanya wa kuwapigia simu mapaparazi ambapo ndani ya muda mfupi walifika na kumshuhudia Dina akiwa ndani ya Bajaj huku akivaa nguo kabla ya kumuamuru dereva kuondoka kwa spidi.
Naye mwanaume ambaye alikuwa ndani ya chumba cha gesti hiyo, aliposikia waandishi wamefika, alitokea mlango wa nyuma akiwa amevaa ‘boksa’ na tisheti, akaacha suruali yake chumbani hapo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi huku akiwaonesha mapaparazi kitanda kilichokuwa vululuvululu, kilichotumika katika usaliti huo pamoja kondom, Flaviana alisema: “Nimeumia sana, yaani nimesalitiwa nikiwa humuhumu chumbani, Aron kanidhalilisha sana na huyo Dina naye kumbe siyo mtu, nitahakikisha namsaka nimshikishe adabu.”Posted by www.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment