LEO
huko Arena Fonte Nova, Mjini Salvador, Wenyeji Brazil wanapambana na
Italy katika Mechi ya mwisho ya Kundi A la Mashindano ya FIFA ya Kombe
la Mabara huku Timu zote zikiwa tayari zimeshatinga Nusu Fainali.
Spain wameshatinga Nsu Fainali toka
Kundi B na Timu nyingine itakayoungana nao itaamuliwa hapo kesho wakati
wa Mechi za mwisho za Kundi B zitakapochezwa.
Leo, kwenye Kundi A ipo Mechi nyingine
ambayo itaanza wakati sawa na ile ya Brazil v Italy ambayo ni kati ya
Japan na Mexico, Mechi ambayo ni ya kukamilisha Ratiba tu kwani Timu
hizi zote mbili zimeshatolewa nje ya Mashindano.
BRAZIL V ITALY
Katika Mechi hii, huku Timu zote zikiwa
sawa kwenye Kundi A kwa kuwa na Pointi 6 kila mmoja lakini Brazil wako
juu kwa Ubora wa Magoli, Brazil wanahitaji Sare tu ili kumaliza Vinara
na hivyo kucheza Nusu Fainali dhidi ya Timu ya Pili ya Kundi B.
Brazil wanaweza kucheza Mechi hii bila ya Senta Hafu wa Chelsea, David Luiz, ambae alivunjika Pua walipocheza Juzi na Mexico.
Ingawa Mchezaji huyo ameruhusiwa kucheza
Mechi hadi mwisho wa Mashindano haya na kisha kufanyiwa operesheni,
inawezakana Kocha Luis Felipe Scolari akampumzisha Luiz na kumchezesha
Senta Hafu wa Bayern Munich, Dante.
Italy, chini ya Kocha Cesare Prandelli,
watalazimka kufanya mabadiliko mawili kwa kumkosa Mkongwe wao Andrea
Pirlo, ambae ana maumivu ya Mguu, na pia Kiungo wa AS Roma, Daniele De
Rossi, ambae yupo Kifungoni baada kupata Kadi ya Njano ya Pili
walipoifunga Japan hapo Juzi.
Akiongelea mpambano huu, Kocha Cesare Prandelli, amesema: “Brazil wana Wachezaji imara, wenye nguvu na Mafowadi wanne hatari!”
Mafowadi hao wanne wa Brazil ni Neymar, Fred, Hulk na Jo.
Katika Mashindano haya, Brazil wamezichapa Japan 3-0 na Mexico 2-0 wakati Italy imezifunga Mexico 2-1 na Japan 4-3.
-Brazil na Italy zimekutana mara 15 kwa Brazil kushinda 7 Italy mara 5 na Sare 3.
-Mara ya mwisho kucheza ni Mechi ya
Kirafiki huko Geneca, Uswisi Mwezi Machi na kutoka Sare 2-2 baada ya
Brazil kuongoza 2-0 kwa Bao za Oscar na Fred na Italy kusawazisha
Kipindi cha Pili kwa Magoli ya Daniele De Rossi na Mario Balotelli.
VIKOSI VNATARAJIWA:
BRAZIL: (Mfumo: 4-2-3-1) Julio Cesar; Alves, Thiago Silva, Dante, Filipe; Gustavo, Hernanes; Hulk, Oscar, Neymar; Jo.
ITALY: (Mfumo: 3-5-1-1) Buffon; Barzagli, Bonucci, Chiellini; Abate, Marchisio, Montolivo, Aquilani, De Sciglio; Giaccherini; Balotelli.
MSIMAMO:
KUNDI A | |||||||||
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Brazil | 2 | 2 | 0 | 0 | 5 | 0 | 5 | 6 |
2 | Italy | 2 | 2 | 0 | 0 | 6 | 4 | 2 | 6 |
3 | Japan | 2 | 0 | 0 | 2 | 3 | 7 | -4 | 0 |
4 | Mexico | 2 | 0 | 0 | 2 | 1 | 4 | -3 | 0 |
KUNDI B | |||||||||
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Spain | 2 | 2 | 0 | 0 | 12 | 1 | 11 | 6 |
2 | Nigeria | 2 | 1 | 0 | 1 | 7 | 3 | 4 | 3 |
3 | Uruguay | 2 | 1 | 0 | 1 | 3 | 3 | 0 | 3 |
4 | Tahiti | 2 | 0 | 0 | 2 | 1 | 16 | -15 | 0 |
RATIBA/MATOKEO:
Juni 15
Brazil 3 Japan 0
Juni16
Mexico 1 Italy 2
Spain 2 Uruguay 1
Juni 17
Tahiti 1 Nigeria 6
Jumatano Juni 19
Brazil 2 Mexico 0
Italy 4 Japan 3
Alhamisi Juni 20
Spain 10 Tahiti 0
Nigeria 1 Uruguay 2
Jumamosi Juni 22
Saa 4 Usiku
Japan v Mexico [Belo Horizonte]
Italy v Brazil [Salvador]
Jumapili Juni 23
Saa 4 Usiku
Nigeria v Spain [Fortaleza]
Uruguay Tahiti [Recife]
NUSU FAINALI
Jumanne Juni 26
[Belo Horizonte]
[SAA 4 USIKU]
Mshindi A v Mshindi wa Pili B
Jumatano Juni 27
[Fortaleza]
[SAA 4 USIKU]
Mshindi B v Mshindi wa Pili A
MSHINDI WA TATU
Jumapili Juni 30
[Salvador]
[SAA 1 USIKU]
FAINALI
Jumapili Juni 30
[Rio De Janeiro] posted by www. Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment