Sunday, June 23, 2013

GUARDIOLA & BAYERN: KAZI SASA IMEANZA, KIMBEMBE CHA KWANZA KWA PEP NI JULAI 24 NA BARCA!!

PEP_GUARDIOLABAYERN_MUNICH_LOGO
KOCHA MPYA wa Bayern Munich, Mabingwa wa Ulaya na Germany, Pep Guardiola, sasa anaanza rasmi kibarua chake kwa kuzungumza na Wanahabari hapo kesho Jumatatu.

JULAI 27 GERMAN SUPER CUP: BAYERN v DORTMUND!
AGOSTI 9 BUNDESLIGA INAANZA!!
AGOSTI 30 UEFA SUPER CUP: BAYERN v CHELSEA!!
Guardiola, ambae alikuwa Kocha wa FC Barcelona kabla kuondoka, aliteuliwa kuwa Kocha wa Bayern Munich Miezi 6 iliyopita na sasa ana kibarua kipya cha kuiletea Bayern Munich mafanikio yale yale ambayo aliipa Barcelona alipokuwa nao kwa Miaka minne na kutwaa Vikombe 14.
Lakini safari hii kibarua hiki kinaonekana kigumu maana anairithi Bayern Munich iliyokuwa chini ya Kocha Jupp Heynckes ambae Msimu uliokwisha Mwezi Mei aliiongoza vyema na kuweka Historia kwa kutwaa Trebo-Ubingwa wa Germany, Kombe la Germany na Kombe la Ubingwa wa Ulaya.
Guardiola, mwenye Miaka 42, anakabiliwa na changamoto kadhaa huko Germany kubwa ikiwa Bayern Siku zote inategemewa kuwa Bingwa na ikiukosa basi lazima iwemo 3 bora ili kucheza Ulaya kwenye UCL, UEFA CHAMPIONZ na Kocha anaekosa hayo ni wazi kibarua hana tena.
Changamoto nyingine kwa Pep Guardiola ni lugha lakini inadaiwa tangu alipoteuliwa kuwa Kocha wa Bayern, alikuwa akiishi huko New York, Marekani na alikuwa akijifunza Kijerumani kwa Masaa manne kwa Siku.
Akiongelea kuhusu Kocha huyo mpya, aliekuwa Rais wa Bayern, Franz Beckenbauer, alieiongoza Germany kama Nahodha na Kocha kutwaa Ubingwa wa Dunia, amesema: “Mwanzoni mambo yatakuwa magumu kwake. Lazima apindue mafanikio ya Jupp Heynckes ambayo ni magumu kuyafikia labda atwae Klabu Bingwa Duniani Mwezi Desemba!”
Hata hivyo, Guardiola ana nafasi kubwa ya kutwaa mafanikio ya haraka mara baada ya kuanza kazi yake kwani Jumatano hii inayokuja ndio anaanza Mazoezi rasmi na Wachezaji wake ndani ya Allianz Arena ambako Washabiki wao 25,000 wataruhusiwa kuingia kuiona Timu yao.
Julai 24, Barcelona watatua Munich kucheza Mechi ya Kirafiki na Bayern na Julai 27 Bayern wanaivaa Borussia Dortmund kugombea German Super Cup.
Agosti 9, Bayern wanaanza rasmi utetezi wao wa Taji lao la Bundesliga kwa kucheza na Borussia Moenchengladbach.
Agosti 30, Bayern wanaivaa Chelsea, ambayo iliwatoa kwenye Fainali ya UCL Mwaka 2012, na safari hii wanagombea UEFA Super Cup Mjini Prague, Czech Republic.
Desemba ndio Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani na Bayern Munich watawakilisha Bara la Ulaya.
Akifanikiwa kuvuka vizingiti vyote hivyo, bila shaka, Pep Guardiola atakuwa njiani kuleta mafanikio yake alipokuwa Barcelona kwa Bayern Munich.Posted bywww. Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment