Friday, June 28, 2013

KLABU ZALILIA ZAWADI ZAO ZA LIGI!! MAKUBWA YASEMWA




YANGA_MJENGO

WAKATI inasemekana TFF walishalipwa Shilingi Milioni 200 toka kwa Wadhamini wa Ligi Kuu ya Bara, VODACOM, tangu Mwezi uliopita zikiwa ni Zawadi kwa Washindi mbali mbali wa Ligi hiyo, Klabu zimelalamika kutolipwa Zawadi zao na Yanga wametaka walipwe Milioni 70 zao kabla Jumapili.

Zawadi hizo ni kwa ajili ya kumtunukia Bingwa, Yanga, pia wengine wanaostahili ni ni Azam FC, Simba, Kagera Sugar pamoja na Wachezaji mbali mbali wakiwemo Kipa Bora, Mfungaji Bora, ambae ni Kipre Tcheche wa Azam FC, Refa Bora, Kocha Bora na kadhalika.
Hata hivyo, Vodacom inasemekana wameshatangaza Zawadi hizo zitagawiwa mapema Mwezi ujao na hilo limegusiwa pia na TFF ambao wamesema wanaandaa Siku maalum ya kutoa Zawadi hizo ikiwa ni pamoja na kualika Maafisa wa Serikali pamoja na wale kutoka Wizara husika hasa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Msimu uliopita hata Simba walicheleweshwa kupata Zawadi yao kama Bingwa baada ya kusubiri karibu Miezi miwili tangu Ligi imalizike ili kupata Tuzo yao.
Yanga walitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2012/13 uliomalizka Mwezi Mei lakini wao walitwaa Ubingwa huo mapema kabla Msimu huo haujafika tamati. 
YANGA YAITAKA TFF IWALIPE KABLA JUMAPILI!!

0 comments:

Post a Comment