“Baba
ameondoka tangu Mei (mwaka huu) na kwenda Umalila, Mbeya Vijijini
ambako inasemekana ameoa mwanamke mwingine,” alisema Agustino......................................
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watoto wawili wa kike na kiume
wanaoishi katika Mtaa wa Jacaranda, Airport jijini Mbeya, wenye umri wa
miaka 7 na 8 wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi mitano bila
ya kupata huduma kutoka kwa wazazi wao.
Wazazi
hao ambao majina yao hayakupatikana, wamewaacha watoto hao, Agustino
Steven (8) na Rebeca Steven (7) wanaosoma darasa la kwanza katika Shule
ya Msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela jijini hapa na kwenda kuolewa
na kuoa mbele ya safari.
Mbaya zaidi, watoto hao wameachwa katika
nyumba ya kupanga wakati wakiwa na umri ambao hawawezi kulipa kodi ya
nyumba, hivyo kuishi kwa busara za mwenye nyumba hiyo.
“Baba
ameondoka tangu Mei (mwaka huu) na kwenda Umalila, Mbeya Vijijini
ambako inasemekana ameoa mwanamke mwingine,” alisema Agustino.
Mtoto
huyo aliendelea kudai kwamba baada ya muda, mama yao naye aliondoka
kwenda Mbozi ambako inasadikika kuwa ameolewa na mwanaume mwingine.
Hata
hivyo, pamoja na kuishi katika nyumba hiyo, watoto hao hawakuwa na budi
kujitafutia riziki kwa kuzoa takataka kutoka kwenye nyumba za majirani
na kuzipeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500.
Baada ya kuulizwa kwa nini wanafanya kazi hiyo, ndipo Agustino na Rebeca
walipofunguka na kutoa simulizi ya kusikitisha kwa kudai kwamba
walikuwa wakijitahidi kutafuta fedha angalau wawe wanakula mlo mmoja kwa
siku.
“Mara
nyingi asubuhi huwa tunaenda shule bila kunywa chai, hela tunazozipata
kwa kuzoa takataka zinatusaidia kununua unga na mboga na kujipikia mlo
wa usiku,” alisema Rebeca.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mwenyekiti
wa Dawati la Jinsia lililopo chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo
amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji
watoto hao.
Mwenyekiti huyo amewaomba majirani na wananchi
kuwasaidia polisi ili kuweza kuwabaini wazazi wa watoto hao sehemu
walipo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
“Majirani
wanatakiwa kuwahudumia watoto hao mpaka wazazi wao watakapopatikana na
kuhakikisha wanaendelea na masomo kama kawaida,” alisema Gumbo.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu, umebaini kwamba wazazi hao
waliwahi kumwacha binti yao mwenye umri wa miaka 17 aliyefahamika kwa
jina la Salome Steven kwa kutompeleka shule na kumpa jukumu la kuwalea
wadogo zake hao.
Kutokana
na ugumu wa maisha na harakati za kutafuta fedha kwa ajili ya wadogo
zake, binti huyo aliishia kupachikwa mimba na kuwakimbia wadogo zake,
akaenda kuishi kwa rafiki yake.
Posted by http://thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment