Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa
timu za Cosmopolitan na Taifa Stars, Mathias Kissa (84) kilichotokea
leo alfajiri (Juni 24 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) jijini Dar es Salaam.
Baadaye alijiunga na Cosmoplitan ya Dar
es Salaam, na pia kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambapo enzi zake akiwa
na wachezaji kama Yunge Mwanansali wakiiwakilisha Tanganyika na baadaye
Tanzania Bara walitamba katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati huo
ikiitwa Gossage, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Kissa ambaye alipata tuzo ya mchezaji
bora wa karne kwa upande wa Tanzania, tuzo inayotambuliwa na Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) alikuwa ndiye mchezaji msomi
kupita wote wakati akichezea timu ya Taifa akiwa amehitimu elimu ya
Darasa la Kumi.
Kwa mujibu wa binti yake, Erica,
marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alioupata
miaka mitano iliyopita, na kisukari. Baadaye alipata kidonda ambacho
ndicho kilichosababisha kifo chake.
Msiba uko nyumbani kwa marahemu, Masaki,
Mtaa wa Ruvu karibu na Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Maziko
yatafanyika keshokutwa, Jumatano (Juni 26 mwaka huu) kwenye makaburi ya
Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu
Kisa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya
Cosmopolitan na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki
kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Kisa mahali
pema peponi. Amina
KIUNGO wa Simba, Amri Kiemba, ndie
lietwaa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Msimu uliopita iliyotolewa na Soccer
Players' Union of Tanzania (SPUTANZA) katika Tamasha maalum
lililofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam Jumamosi
Usiku.
Hili ndio Tamasha la kwanza kwa SPUTANZA kuandaa na kutoa Tuzo za aina hii.
Kiemba alizoa Asilimia 47.88 ya Kura zilizopigwa na Makocha na Manahodha wa Klabu za LigI Kuu Vodacom.
Ni Makocha na Manahodha 17 kati ya 28
ndio waliohudhuria Tamasha hilo wakati ilitarajiwa watakuwepo Kocha na
Nahodha wake kwa kila Timu toka Klabu 14 za Ligi Kuu Vodacom.
Katika uchaguzi wake, Kiemba aliwabwaga Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu na Paul Nonga.
Kwenye Tuzo ya Mchezaji Kijana Bora,
Kiungo wa Azam FC Salum Abubakar aliwabwaga Shomari Kapombe (Simba),
Issa Rashid (Mtibwa) na Hassan Dilunga (JKT Ruvu).
Mshindi wa Kipa Bora alikuwa ni Kipa wa
Mtibwa Sugar, Hussen Shariff, aliewashinda Kipa wa Simba Juma Kaseja na
Mwadini Ally wa Azam FC.
Nae Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime,
alitwaa Tuzo ya Kocha Bora kwa kumshinda Abdallah Kibaden ambae alikuwa
Kocha wa Kagera Sugar ingawa sasa yuko Simba pamoja na Jumanne Chale.
Akiongelea uteuzi wa Wagombea Tuzo hizo,
Katibu wa SPUTANZA, Said George, alisema wao walitumia Takwimu
walizopewa na TFF, Shirikisho la Soka Tanzania na pia alielezea
kuridhika kwao na uendeshwaji na mafanikio ya Tamasha lao hilo la kwanza
na kuahidi kuliboresha zaidi kwa Msimu ujao.posted by www,Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment