STAA
Lionel Messi ameripotiwa kulipa kiasi cha ziada ya Kodi kwa Miaka ya
2010 na 2011 huko Nchini Spain ambacho ni Euro Milioni 10.
Inasemekana malipo haya ya sasa yamelipwa kama Marekebisho ya Kodi zake za Mwaka 2010 na 2011 ambazo alishalipia.
Pia, Messi anatafuta suluhu na Ofisi ya
Kodi kuhusu malipo halali anayopaswa kulipa kwa Miaka ya 2007, 2008 na
2009 na inaaminika kuwa Staa huyo ameshakubali kulipia Kodi Nchini Spain
inayohusiana na Mauzo ya Picha na Matangazo ambayo yalikuwa yakilipwa
Kampuni zake nje ya Spain.
Hapo Juni 12, Ofisi ya Kodi ya huko
Mjini Barcelona ilifungua Mashitaka Mahakamani ikimtuhumu Messi na Baba
yake Mzazi kuhadaa na kukwepa kulipa Kodi za Miaka ya 2007, 2008 na 2009
ambayo Jumla yake ni Euro Milioni 4 kwa kutumia Kampuni zilizo nje ya
Spain.
Messi na Baba yake wametakiwa kufika Mahakamani hapo Septemba 17 huko Gava, karibu na Barcelona, ili kujibu Mashitaka.
Wanasheria wa Staa huyo pamoja na mwenyewe wamedai wao Siku zote wametii na kufuata Sheria zote za Spain.WWW.Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment