Wednesday, June 12, 2013

KOMBE LA DUNIA 214: MASCHERANO ALA NYEKUNDU!!

COLOMBIA YAINYUKA PERU 2-0, FALCAO ATIKISA KAMBA!!
MESSI_IN_ARGENTINAKITIMTIM cha kwenda Nchi Jirani Brazil Mwaka 2014 kimeendelea huko Marekani ya Kusini katika Mechi za Kundi lao kusaka 4 za kuingia Fainali ya Kombe la Dunia na Ecuador, wakicheza Nyumbani Mjini Quito, Estadio Olímpico Atahualpa, waliiendesha mchakamchaka Argentina na nusura waifunge.
Argentina, katika mara mbili zao walizocheza mwisho huko Quito, wamefungwa Mechi zote na leo waliponea chupuchupu licha ya kupata Bao la awali la Penati ya Dakika ya 4 iliyofungwa na Sergio Aguero baada ya Dominguez kumuangusha Palacio ndani ya Boksi.
Dakika 13 baadae, Ecuador walisawazisha Bao hilo kupitia Segundo Castillo.
Ecuador 1
-Dakika ya 17 Segundo Castillo
Argentina 1
-Dakika ya 4 Sergio Aguero [Penati]
-KADI NYEKUNDU: Dakika ya 86 Javier Mascherano
Kwenye Dakika ya 61 Argentina walimpumzisha Sergio Aguero na kumuingiza Lionel Messi lakini ni Ecuador ndio walibaki juu na kukosa Bao kadhaa.
Katika Dakika ya 86, Javier Mascherano, wakati akitolewa nje kwenye Kigari cha Machela, alionyeshwa Kadi Nyekundu kwa madai ya kumpiga teke Mtoa Huduma ya Kwanza kwenye Kigari hicho.
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Argentina
13
7
5
1
25
9
16
26
2
Colombia
12
7
2
3
21
7
14
23
3
Ecuador
12
6
3
3
17
12
5
21
4
Chile
12
6
0
6
18
20
-2
18
5
Venezuela
12
4
4
4
10
13
-3
16
6
Peru
12
4
2
6
12
17
-5
14
7
Uruguay
11
3
4
4
17
21
-4
13
8
Bolivia
12
2
4
6
14
21
-7
10
9
Paraguay
12
2
2
8
9
23
-14
8
**FAHAMU: Timu 4 za Juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka Kanda ya ASIA kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.
Katika Mechi nyingine iliyoanza mapema, Colombia wamezidi kuiandama Argentina kileleni baada ya kuichapa Peru Bao 2-0 kwa Bao za Dakika ya 13 kwa Penati ya Radamel Falcao Garcia na Dakika ya 45 kupitia Teofilo Gutierrez.
Peru walimaliza Mechi hiyo kwa kuwa Mtu 10 baada ya Carlos Zambrano kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 70.
Timu 4 za Juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka Kanda ya ASIA kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.
VIKOSI VILIVYOANZA:
ECUADOR: Dominguez, Paredes, Guagua, Erazo, Ayovi; Valencia, Noboa, Castillo, Montero; Caicedo, Rojas.
ARGENTINA: Romero; Peruzzi, Fernandez, Garay, Basanta, Rojo; Banega, Mascherano, Di Maria; Palacio, Agüero.
RATIBA/MATOKEO:
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumanne Juni 11
Ecuador 1 Argentina 1
Colombia 2 Peru 0
Jumatano Juni 12
03:00 Venezuela v Uruguay [1-1]
03:30 Chile v Bolivia [2-0]
Jumapili Septemba 8
01:00 Colombia v Ecuador [0-1]
01:00 Chile v Venezuela [2-0]
01:00 Paraguay v Bolivia [1-3]
01:00 Peru v Uruguay [2-4]
Jumanne Septemba 10
03:00 Bolivia v Ecuador [0-1]
03:00 Paraguay v Argentina [1-3]
0300  Venezuela v Peru[1-2]
03:00 Uruguay v Colombia [0-4]

0 comments:

Post a Comment