Tuesday, February 25, 2014

Tazama Mbinu za kufanikisha elimu kwa mtoto wa kike


Kwa kuwa watoto wa kike nao wana haki ya kuhitimu masomo kama ilivyo kwa wenzao wa kiume, chapisho lingine la HakiElimu liitwalo: Mbinu za kufanikisha elimu kwa wasichana
,............................ linapendekeza njia kadhaa za kuwanusuru wasichana ili hatimaye watimize ndoto za maisha yao. Chapisho linaeleza:
Wazazi na walezi kuwajengea watoto wa kike msingi mzuri wa malezi kwa kuongea nao na kuwaelekeza.
Tunaweza kuwajengea uwezo wasichana kutambua uwezo wao ili kujijengea msingi mzuri katika maisha yao, kwa kuwapa maadili ya msingi tangu wakiwa wadogo.
Kaya masikini ziwezeshwe kwa mitaji midogo midogo, mikopo, ruzuku za kilimo na kupunguziwa ushuru.
Mbinu hii itasaidia kupunguza makali ya umaskini kwa kaya zenye maisha duni. Watanzania ni wachapakazi, iwapo watawezeshwa wataweza kujiingizia kipato kitakachowawezesha kuwapatia watoto wao elimu.
Watoto wa kike wasome kwenye shule zilizo karibu na maeneo wanayoishi.
Hili litapunguza tatizo la wasichana kuacha shule na kupunguza uwezekano wa kupata vishawishi na vikwazo vya kielimu. Wazazi wanaowaandikisha watoto wa kike shule za mbali, hawana budi kuacha maana ni kuwajengea mazingira ya kupata vikwazo zaidi kimasomo..
Shule za mbali ziwe na mabweni kwa wasichana
Hili litapunguza tatizo la wasichana kuacha shule, hasa sehemu za vijijini ambako wasichana wanalazimika kutembea umbali mrefu. Wakijengewa mabweni itawasaidia kufanikisha masomo yao.
Wasichana waliopevuka wapewe elimu ya uzazi kwa uwazi zaidi
Kama wasichana wataelewa kuhusu mabadiliko yao kimakuzi na elimu ya uzazi kwa jumla, watakuwa wanajua wanachokifanya wakati wote, hivyo itakuwa rahisi sana kwao kujiepusha na vitendo vya ngono, pia kujikinga na mimba za utotoni zinazowagharimu elimu yao na afya zao.
Umuhimu wa kuendelea kuelimisha na kuhamasisha kuachana na mila kinzani zinazowaandaa wasichana kufeli maisha yao.posted by thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment