Tuesday, June 17, 2014

BRAZIL YASHIKWA PABAYA,

BRAZIL_v_MEXICO-NEYMAR 














Mechi za Pili kwa Kundi A la Fainali za Kombe la Dunia zimeanza Leo Estadio Castelão, Fortaleza na Wenyeji Brazil kutoka Sare ya 0-0.

Sare hii imeibakisha Brazil juu kwenye Kundi wakiwa na Pointi 4 sawa na Mexico.
Wakati Kipindi cha Kwanza kilikuwa vuta ni kuvute ingawa Neymar alikosa Bao la Kichwa ambacho Kipa Ochoa aliokoa vizuri, Kipindi cha Pili Brazil, hasa mwishoni, walikuja juu mno na kukosa Bao kadhaa huku Kipa Ochoa akiokoa tena na tena na, bila shaka, ndie alieinusuru Mexico.
Jumatano ni zamu ya Cameroon na Croatia kucheza Mechi zao za Pili za Kundi A baada ya wote kupoteza Mechi zao za kwanza.
Mechi ya mwisho Brazil watacheza na Cameroon huko Nacional, Brasilia Jumatatu Juni 23 na wakati huo huo Mexico kuivaa Croatia.
VIKOSI:
BRAZIL: Julio Cesar; Dani Alves, Thiago Silva, David Luiz, Marcelo; Paulinho, Gustavo; Ramires, Oscar, Neymar; Fred
Akiba: Jefferson, Fernandinho, Hulk, Dante, Maxwell, Henrique, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Maicon, Victor.
MEXICO: Ochoa; Aguilar, Rodriguez, Marquez, Moreno, Layun; Herrera, Vazquez, Guardado; Giovani, Peralta

Akiba: Corona, Salcido, Reyes, Fabian, Jimenez, Pulido, Hernandez, Ponce, 
Brizuela, Aquino, Pena, Talavera.

REFA: Cuneyt Cakir (Turkey)
KOMBE LA DUNIA
MSIMAMO:
KUNDI A
TIMU P W D L F A GD PTS
Brazil 2 1 1 0 3 1 2 4
Mexico 2 1 1 0 1 0 1 4
Cameroon 1 0 0 1 0 1 -1 0
Croatia 1 0 0 1 1 3 -2 0
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
JUMANNE, JUNI 17, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Belgium 2 Algeria 1 H Estadio Mineirão
2200 Brazil 0 Mexico 0 A Estadio Castelão
0100 Russia v South Korea H Arena Pantanal
JUMATANO, JUNI 18, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Australia v Netherlands B Estadio Beira-Rio
2200 Spain v Chile B Estadio do Maracanã
0100 Cameroon v Croatia A Arena Amazonia
ALHAMISI, JUNI 19, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Colombia v Ivory Coast C Nacional
2200 Uruguay v England D Arena Corinthians
0100 Japan v Greece C Estadio das Dunas

0 comments:

Post a Comment