JAJI
wa Mahakama huko Nchini Spain ametoa samansi ya kumtaka Nyota wa
Barcelona Lionel Messi awepo Mahakamni Septemba 17 kuhusiana na tuhuma
za udanganyifu ili kukwepa kulipa Kodi.
Messi na Baba yake wamekana tuhuma hizo.
Inaaminika Mshahara wa Messi kutoka
Klabu yake Barcelona ni kiasi cha Euro Milioni 16 kwa Mwaka, kipato
ambacho kinamfanya awe mmoja wa Wanamichezo wanaolipwa Fedha nyingi
Duniani.
Pia, Messi ana Mikataba kadhaa wa kadha na Wadhamini wakubwa Duniani inayomuingizia Mamilioni ya Fedha.
Inadaiwa Messi na Baba yake, Jorge,
wanahutumiwa kuhadaa mara 3 ulipaji wa Kodi halali kwa Serikali ya Spain
na Mapato yanayohusishwa na tuhuma hizo ni yale yanayohusiana na
uuzwaji wa Picha zake katika Mikataba yake na Kampuni za Banco Sabadell,
Danone, Adidas, Pepsi-Cola, Proctor and Gamble na Kuwait Food Company.
Ikiwa atapatikana na hatia Messi anaweza kupewa Kifungo cha Miaka 6 Jela pamoja na Faini kubwa juu.
Akizungumzia tuhuma hizo kwenye Ukurasa
wake wa Mtandao wa Facebook, Messi aliandika: “Hatujafanya kosa lolote.
Daima tumekuwa tukitimiza wajibu wetu katika majukumu yetu ya Kodi.”
Mafanikio ya Messi katika Soka yamemfanya Mchezaji huyo awe na Soko kubwa la uuzwaji wa Picha zake na Matangazo.
Messi ni Mchezaji alietokea kwenye
Familia ya kimasikini na alijiunga na Barcelona akiwa na Miaka 13 hapo
Mwaka 2000 na kuanza kuichezea Timu ya Kwanza Miaka mitatu baadae.
Rais wa Barcelona, Sandro Rosell, amesema Klabu yao haina wasiwasi kuwa Nyota wao hana hatia ya kukwepa Kodi.Posted by Www.Thesuperonenews.bolgspot.com
0 comments:
Post a Comment