
Mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Old
Trafford dhidi ya Sevilla ya Spain hapo Agosti 9 ikiwa ni Siku mbili tu
kabla ya Man United kucheza Uwanja wa Wembley katika ile Mechi ya
kufungua pazia ya Msimu mpya watakapokutana na Wigan Athletics ambao
ndio Mabingwa wa FA CUP hapo Agosti 11.
Mwenyewe Rio Ferdinand amenena: “Hii
Klabu ni ya kipekee kwa kila hali, historia yake na msukumo wake huwezi
kuamini, unamfanya kila Mtu apiganie kufanikiwa!”
Aliongeza: “Usiku huo utakuwa mkubwa
kwangu na utatikisa mawazo yangu! Siamini kama Miaka 10 imepita na nina
bahati kuitumikia Man United! Mashabiki wetu ni bora Dunia nzima, wana
mapenzi na ninashkuru kwa sapoti yao. Natumai watapata raha Usiku huo!”
Sir Alex Ferguson, ambae alimsaini
Ferdinand Mwaka 2002 toka Leeds United, alisema: “Ni kitu muhimu kwa
Klabu kuweka Mechi hii spesho kwa Utumishi wake! Yeye ni mmoja wa Mabeki
bora Klabu hii imepata kuwa nao! Rio ana kipaji cha asili cha kusoma
Mchezo na Mwezi uliokwisha nilitamka kwamba naamini Msimu huu ndio
uliokuwa bora katika maisha yake na Man United! Utakuwa Usiku murua
kwake na Mashabiki, na pia ni safi kwa kuanza Msimu mpya namna hii!”
Rio Ferdinand ameichezea Man United Mechi 432 na kutwaa Ubingwa wa England mara 6 na Ubingwa wa Ulaya hapo Mwaka 2008.
0 comments:
Post a Comment