Wednesday, June 12, 2013

MSIMU MPYA 2013/14: LINI KUANZA BPL, LA LIGA, BUNDESLIGA & SERIE A ?


BAYERN_v_BARCELONAMARA BAADA ya LIGI maarufu, LIGI VIGOGO, Barani Ulaya kukamilika na kuzaa Mabingwa wa BPL, Manchester United, La Liga, FC Barcelona, Bundesliga, Bayern Munich, na huko Italy Serie A, Juventus, Wadau sasa wanangojea kwa hamu Msimu ujao wa 2013/14 utakaoanza Agosti.



ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU:
BUNDESLIGA
-Ligi itaanza Tarehe 9 Agosti 2013 na kumalizika 10 Mei 2014

-Mapumziko ya Majira ya Baridi, Winta, ni kati ya Desemba 20, 2013 na 26 Januari 2014.
-Timu 18 kushiriki Ligi hii.
SERIE A
-Ligi itaanza Tarehe 25 Agosti 2013 na kumalizika 18 Mei 2014
-Mapumziko ya Majira ya Baridi, Winta, ni kati ya Desemba 23, 2013 na 5 Januari 2014.
-Kutakuwa na Raundi 3 za Mechi za katikati ya Wiki hapo Tarehe 25 Septemba 2013, 30 Oktoba 2013 na7 Mei 2014.
-Timu 20 kushiriki Ligi hii.
-Fainali ya Kombe la Italy, Coppa Italia au IM Cup 2014 itafanyika Jumatano 16 April 2014
-TIM Supercup 2013 itafanyika huko China Mwezi Agosti 2013.
LA LIGA
-Ligi itaanza Tarehe 17 Agosti 2013 na kumalizika 18 Mei 2014
-Mapumziko ya Majira ya Baridi, Winta, ni kati ya Desemba 8, 2013 na 5 Januari 2014.
-Timu 20 zitashiriki.
-Fainali Copa del Rey 19 Aprili 2014
BPL
-NGAO ya JAMII: 11 Agosti 2013 Uwanja wa Wembley, London Saa 10 Jioni: Mabingwa Manchester United v Wigan Athletics, Washindi wa FA CUP
-Ligi itaanza Tarehe 17 Agosti 2013 na kumalizika 11 Mei 2014
-Mapumziko ya Majira ya Baridi, Winta: Hamna
-Timu 20 kushiriki Ligi hii.
-Ratiba ya Ligi kutolewa Juni 19
-Fainali FA CUP ni Tarehe 17 Mei 2014

0 comments:

Post a Comment