Friday, June 21, 2013

MKOANI MBEYA POLISI WAFANYA KUFURU YA MAUWAJI


                                                                   IGP Mwema
MTU mmoja  Mkazi wa kijiji cha Lumbila Wilayani Mbozi  Mkoani Mbeya,aitwaye Rajabu Wilson (25) ameuwawa na polisi na askari wanne kujeruhiwa vibaya baada ya kuwashambulia ,polisi waliokuwa katika msako wa waharifu katika Mlima Senjele.

Tukio la kuuwawa kwa mwananchi huyo lilifuatiwa baada ya wananchi wa eneo hilo kuwazuia  askari polisi waliokuwa katika msako dhidi ya wahalifu Mlima Senjele kwa kujikusanya kundi kubwa  na kuzingirwa  na wananchi zaidi 150 wa kijiji hicho wakiwa na silaha za jadi mapanga marungu, shoka na mawe kwa lengo la kuwadhulu askari hao.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Bw. Diwani Athuman alisema kuwa tukio hilo limetokea juni 19 mwaka huu majira ya saa 7.00 mchana  katika kijiji cha Lumbila baada ya kukutwa na madumu 100 ya mafuta aina ya Dieseli ya wizi.

 Bw. Athuman alisema kuwa lengo la wananchi hao ni kuwazuia askari hao kukamata wahalifu na kuanza kufanya vurugu baada ya kuwa wamekamata mali inayodhaniwa kuwa ya wizi ambayo ni mafuta  aina ya diesel madumu zaidi ya 100, hata hivyo kufuatia vurugu zilizojitokeza walifanikiwa kuchukua madumu machache ambayo ni madumu matatu yenye ujazo wa lita 60, madumu mawili yenye ujazo wa lita 20 na madumu nane lita 30 kufanya oparesheni. 

 Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa kutokana na vurugu hizo za wananchi ndio uliowafanya askari polisi washindwe kuchukua vielelezo vyote.ambapo licha hiyo waliweza kuchukjua  madumu machache baada ya vurugu kuwa nyingi kutoka kwa wananchi.

 Hata hivyo Diwani Athuman alisema kuwa katika vurugu hizo wananchi walifunga barabara kuu ya mbeya/tunduma kwa kuweka mawe na magogo na kusababisha msongamano mkubwa wa magari barabarani.

 Alisema kuwa hali ya usalama ilianza kuwa shwari kamanda wa polisi kufika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wa eneo hilo kisha kufungua barabara , pia katika tukio hilo  askari polisi wanne walijeruhiwa katika tukio hilo kati yao watatu walipatiwa matibabu na kuruhusiwa na askari mmoja  amelazwa hospitali ya rufaa mbeya kwa matibabu zaidi . 

 Aidha Bw. Athuman ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria badala yake kuwa na utamaduni wa kutatua malalamiko yao kwa njia ya mazungumzo kwa kuyawasilisha katika mamlaka husika.
 
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya katika hospitali ya wilaya ya mbozi kwa uchunguzi ili ndugu zake waweze kukabidhiwa kwa mazishi.Posted by www.Thesuperonews.blgspot.com

0 comments:

Post a Comment