Friday, June 21, 2013

ANGALIA LULU AFURAHIA KUZALIWA KWA KANUMBA MPYA

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu,’ hivi karibuni alionesha kufurahia kuzaliwa kwa mtoto wa wifi yake ambaye ni dada wa marehemu Steven Kanumba aitwaye Abela.

Msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu,’ hivi karibuni alionesha kufurahia kuzaliwa kwa mtoto wa wifi yake ambaye ni dada wa marehemu Steven Kanumba aitwaye Abela.
Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa na Kanumba Jr.
Akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Lulu alionekana amempakata mtoto huyo wa kiume aliyepachikwa jina la Kanumba Jr. huku akichekelea kuashiria amepata mtu wa kujiliwaza naye.
Mbali na Lulu, Mama Kanumba, Flora Mtegoa na Mama lulu, Lucresia Kalugira walikuwa miongoni mwa watu walioshangilia kuzaliwa kwa mtoto huyo ambapo juzi walionekana kituko hospitalini hapo kutokana na furaha ya kupitiliza waliyokuwanayo.posted by Www.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment