Friday, June 7, 2013

MKOANI MBEYA MAHAFALI YA KUMALIZA KOZI NAMBA 20 YA DALAJA LA KWANZA NGAZI YA ASKARI MAGEREZA YAFANYIKA LEO


Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akipokea Salamu za heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
 KWA PICHA ZAID ENDELEA KUSOMA
 
 Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akikagua wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
 Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheo cha Ukoplo Askari B4448 Patric Babara kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
 Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti muhitimu B7348 Patrick Chalemta  aliye fanya vizuri masomo ya Darasani katika  mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20
  Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti muhitimu aliye fanya vizuri somo la kulenga shabaha 3163 Tatu Amri  katika  mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 
  Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimpa zawadi  muhitimu 3914 Leonida Hillu ya mwnafunzi mwenye Nidhamu usafi na ukakamavu katika  mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20
 Baadhi ya Maofisa wakitoa heshima katika mahafali ya mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
 Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga (kushoto) akiwa na Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira Staniford Ntirudura wakipokea Salamu za heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
 Wahitimu wakiwa kwenye Gwaride  wakipita kwa mwendo wa Haraka mbele ya Mgeni Rasmi.
 "Hima..... Hima.... Hima!.... " Ni salamu ya utii ikiongozwa na Parade Kamanda SP Lucas Ndoteela
 Baadhi ya Maofisa wakifuatilia kwa Makini shughuli za Mahafali
 Baadhi ya Wahitimu wakionesha umahili wa kupambana na maadui
 Watoto wanaolelewa na kituo cha malezi ya watoto wadogo katika chuo cha Magereza wakitumbuiza katika Sherehe za Mahafali
 Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishina msaidizi wa Magereza  Staniford Ntirudura akizungumza jambo katika mahafali hayo.
 Wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya, wakifuatilia matukio yanayo endelea katika Sherehe zao.
 Wahitimu B5414 Peter Ndalahwa na 3469 Matha Mwanjala wakisoma Lisara katika mahafali yao
 Muhitimu B3494 Willy Timoth akisoma Shairi wakati wa mahafali
 Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akizungumza na wahitimu

********************
JUMLA ya Askari 984 wa Jeshi la Magereza, wanaume 845 na wanawake 139  wametunukiwa  Vyeo vya Ukoplo baada ya kuhitimu mafunzo ya Uongozi daraja la Kwanza kozi namba 20 katika Chuo cha Magereza Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Vyeo hivyo vilitolewa na Kamishina wa Fedha na Utawala Gaston Sanga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho leo Juni 7, Mwaka huu.
Akizungumza katika mahafali hayo, Kamishina wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga amesema Askari wa Jeshi la Magereza Nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, taratibu na kanuni za kazi kwa kufuata uwajibikaji, unyenyekevu, ukakamavu, ujasili, upendo, ushirikiano, uvumilivu, uaminifu na nidhamu.
Kamishina Sanga amesema Maaskari wanapaswa kuzingatia elimu waliyopewa wakati wa mafunzo ili wakawe mfano kipindi cha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwaongoza wenzao ambao hawakupatiwa elimu kama yao.
Aidha amewaasa kutowatesa Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia kwa kuzingatia kuwa wanamhudumia binadamu kama walivyo wao  na siyo kuchukua nafasi ya kuwanyanyasa bila kuogopa haki na Stahili za binadamu japokuwa ni wafungwa.


0 comments:

Post a Comment