
Akihojiwa na kwenye Shoo ya TV, Punto
Pelota, huko Spain, Mourinho, ambae ataanuliwa rasmi kuwa Meneja mpya wa
Chelsea Jumatatu ijayo, akielezea jinsi uhusiano wake na Ronaldo
ulivyoyumba Msimu uliopita, alinena: “Nilikuwa na tatizo moja tu na
Ronaldo. Tatizo dogo na rahisi tu ambalo Kocha akimlaumu Mchezaji ili
kuboresha mbinu za Timu, Mchezaji huchukia. Wakati huo alikuwa
hakubaliani na hilo labda kwa vile anajiona anajua kila kitu na Kocha
hawezi kumuendeleza chochote!”
Mourinho aliongeza: “Cristiano alikuwa
na Misimu mitatu mizuri na mimi. Sijui kama ilikuwa ndio bora kwake
kwani akiwa na Manchester United alipata mafanikio makubwa! Lakini
nadhani, kimbinu, tulimtengenezea hali nzuri ya kumfanya atumie kipaji
chake kuweka rekodi na kufunga Bao nyingi!”
Baada kuondoka Mourinho, zipo tetesi
nzito kuwa nae Ronaldo anataka kuondoka Real huku Man United ikitajwa
sana pamoja na Chelsea.
Hata hivyo, Rais wa Real, Florentino Pérez, hivi Juzi alisisitiza Ronaldo haendi popote.
0 comments:
Post a Comment