Wednesday, June 12, 2013

JEZI YAMPA WASIWASI PAPISS CISSE IKAWA NEWCASTLE

STRAIKA wa Newcastle Papiss Cisse yupo kwenye hali ngumu ya kuvaa Jezi ya Klabu yake Newcastle ambayo sasa Mdhamini wake ni Kampuni ya Mikopo kitu ambacho ni kinyume na imani yake ya Kiroho.
Cisse, mwenye Miaka 28 na Mchezaji toka Senegal ambae ni Muislamu, ameonya kuwa imani yake hairuhusu kutangaza Kampuni ya kutoa Mikopo kwa Riba.
Cisse:
-UMRI: 28
-UTAIFA: Senegal
-KLABU: Douanes Dakar, Metz, Freiburg & Newcastle
-NEWCASTLE MAGOLI: 26
Msimamo huo pia umedakwa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa huko Uingereza, PFA, Professional Footballers' Association, na Makamu Mkuu wake, Bobby Barnes, amesema hiyo ni hali ngumu lakini anatumaini Klabu ya Cisse itamsaidia.
Cisse alijiunga na Newcastle Januari 2012.
Tatizo kama la Cisse lilimkumba Straika wa Mali Frederic Kanoute wakati akichezea Klabu ya Spain Sevilla Mwaka 2007 wakati Klabu hiyo ilipoingia Mkataba na Kampuni ya Uchezeshaji Kamari wakati Kanoute ni Mwislam.
Imani za Kiislamu zinakataza kabisa Kamari na Kanoute ilibidi acheze huku nembo ya Kampuni hiyo ikiwa imezibwa.

0 comments:

Post a Comment