Thursday, June 6, 2013

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI BRAZIL YAPOROMOKA HADI 22


BRAZIL-LONDONMABINGWA MARA 5 WA DUNIA, Brazil, wameporomoka hadi Nafasi ya 22 katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa leo, hii ikiwa ni Historia, na ukiwa umebaki Mwaka mmoja tu kwa wao kuwa Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014.
Mwezu huu, Brazil wameporomoka Nafasi 3 na hili linachangiwa sana na wao kutoshiriki Mashindano rasmi yanayotambuliwa na FIFA na badala yake kucheza Mechi za Kirafiki ambazo hukusanya Pointi chache katika kukokotoa Ubora wa Timu kwa mujibu wa Mfumo wa FIFA.
Ukokotoaji huo Listi ya FIFA ya Ubora Duniani hutumia Matokeo ya Miaka minne na kwa vile Brazil wao ndio Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia zijazo za Mwaka 2014 wao hawakuhusishwa na Mechi za Mchujo na hivyo kuzikosa Pointi nyingi zinazozolewa na Washiriki wake kwenye mbio za Ubora.
Hata hivyo Brazil wanaweza kupanda Chati ikiwa watafanya vizuri kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yatakayochezwa Nchini kwao kuanzia Juni 15 na kushirikisha Nchi 8 huku wao wakiwa KUNDI A pamoja na Italy, walio Nafasi ya 8 Duniani, Mexico, ya 17, na Japan walio Nafasi ya 32.
MISINGI INAYOTUMIKA KUPATA LISTI YA UBORA DUNIANI:
MECHI:
-Mshindi Pointi 3
-Sare 1
-Kufungwa 0.
UMUHIMU WA MECHI:
-Pointi 4: Kombe la Dunia
-Pointi 3: Fainali za Mabara kama vile COPA AMERICA, EURO, AFCON, Kombe la Mabara
-Pointi 2.5: Mechi za Mchujo Kombe la Dunia au Kombe la Mabara mfano COPA AMERICA, EURO, AFCON
-Pointi 1: Mechi ya Kirafiki
UBORA WA TIMU:
-Nafasi ya Timu kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani hutolewa kwenye 200 na zinazobaki ndio Pointi inazozoa Timu. Kwa mfano Brazil wakicheza na Spain ambao ndio Namba 1 basi 200 TOA 1=199 na hizo ndio Pointi, yaani 199, Brazil atakazozoa akishinda Mechi hiyo.
Mathalani akicheza na Timu iliyo Nafasi ya 100 na kushinda basi 200-100= Brazil atazoa Pointi 100 tu.
NGUVU YA BARA INAKOTOKA TIMU PINZANI:
-Pointi 1: UEFA & CONMEBOL [Nchi za Marekani ya Kusini]
-Pointi 0.88: CONCACAF [Nchi za Marekani ya Kaskazini]
-Pointi 0.86: CAF
-Pointi 0.85: AFC [Asia] [OFC [Oceania]
THAMANI YA MECHI HUPUNGUA KADRI MUDA UNAVYOKWENDA:
-Mechi katika Mwaka mmoja uliopita: Pointi hubaki 100%
-Mechi zilizochezwa nyuma Mwaka 1 hadi 2: Pointi hubaki 50%
- Mechi zilizochezwa nyuma Miaka 2 hadi 3: Pointi hubaki 30%
- Mechi zilizochezwa nyuma Miaka 3 hadi 4: Pointi hubaki 20%
-Mechi zilizochezwa zaidi ya Miaka 4 nyuma: Pointi zote hufutwa 0%
MFANO WA UKOKOTOAJI:
England imecheza na Ukraine [ipo Nafasi 52 kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani] na kushinda Mechi ya Mchujo ya EURO.
-MECHI: Ushindi Pointi 3
-UMUHIMU WA MECHI: Ni Pointi 3 kwa vile ni ya EURO
-UBORA WA TIMU: 200-52=148
-NGUVU YA BARA INAKOTOKA TIMU PINZANI: Pointi 1 [Kwa vile ni ya UEFA]
JUMLA YA POINTI ITAKAZOZOA ENGLAND NI: 3x3x148x1=1332
>>Kwa Ushindi wa Mechi hii ya England v Ukraine, England itazoa Jumla ya Pointi 1332.

0 comments:

Post a Comment