STAA
wa zamani wa Bafana Bafana na Orlando Pirates, Benni McCarthy, Straika
ambae ana sifa ya kipekee ya kuwa Mchezaji pekee aliezoa Tuzo na Mataji
mengi huko Afrika Kusini, ametangaza kustaafu kucheza Soka.
Hivi karibuni, McCarthy alifunga Bao 2
katika Nusu Saa ya mwisho wakati Orlando Pirates inaifunga Golden Arrows
Bao 4–2 na kutwaa tena Ubingwa wa Ligi Kuu huko South Africa.
Ushindi huo ulimaanisha kuwa McCarthy
ndie Mchezaji wa kwanza kutoka South Africa kutwaa Ubingwa wa Ligi mara 3
na Timu 3 tofauti katika Mabara mawili tofauti Duniani kwani ashawahi
kuwa Bingwa pia akiwa Barani Ulaya na Klabu za Ajax Amsterdam ya Holland
na FC Porto ya Portugal.
Kwenye Timu ya Taifa ya South Africa,
Bafana Bafana, Benni, ndie mwenye Rekodi ya kufunga Bao nyingi, akiwa na
Bao 31, na alianza kuichezea Timu hiyo kwenye Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika za Mwaka 1998 ambako alifungana kwa Ufungaji Bora na
Straika hatari wa Misri Hossam Hassan wote wakiwa na Bao 7 na pia yeye
kuteuliwa Mchezaji Bora wa Fainali hizo.
Pia, McCarthy ndie Mchezaji wa kwanza
kutoka South Africa kutwaa UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo alishinda
Mwaka 2004 akiwa na FC Porto.
Akitangaza kustaafu kwake, McCarthy
alinena: “Nimebarikiwa kuwa na maisha ya Soka mazuri yaliyonitoa Viwanja
vya Nyanga Stadium na kuwa Mshindi wa UCL, na Klabu Bingwa Duniani,
hivyo vikiwa ni vilele ambako Mchezaji anaweza kufika akiwa na Klabu!”
Benni McCarthy amesema sasa atakazania kusoma ili afuzu na kupata Beji za Ukocha ili kusaidia Watu wengine.
0 comments:
Post a Comment