Friday, June 21, 2013

ANGALIA PICHA 12 ZA MKE WA MTU ALIYE AMPARAMIA TUNDAMAN JUKWAANI SIKU YA SHOO:

Tundaman baada ya kuangushwa chini na demu huyo.
MSANII wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tundaman’ Jumamosi iliyopita alivamiwa jukwaani na demu wa mtu wakati akitoa burudani kwenye shindano la kumsaka Redd’s Miss Morogoro 2013 ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini humo.…
Tundaman baada ya kuangushwa chini na demu huyo.
MSANII wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tundaman’ Jumamosi iliyopita alivamiwa jukwaani na demu wa mtu wakati akitoa burudani kwenye shindano la kumsaka Redd’s Miss Morogoro 2013 ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini humo.
Demu wa mtu akimfuata Tundaman stejini.
Tundaman aliyepanda jukwaani saa 7 usiku akiwa amechelewa na kusababisha kukorofishana na MC wa shoo hiyo kutokana na kuendelea kutumbuiza hata pale muda wake ulipokuwa umekwisha.
Hata hivyo, mzuka ulikuwa umewapanda mashabiki pamoja na Tundaman na kulazimika msanii huyo kushuka jukwaani na kuanza kucheza na mashabiki wake.
 
...Akiwa stejini na Tundaman.
Tundaman ambaye alionekana kuchangamka kama vile alikuwa ‘ameonja,’ alirudishwa jukwaani na mabaunsa wake  kutokana na kuhofia usalama wake kutoka kwa mashabiki hao.
..
.Akaanza kukata mauno.
Akiwa jukwaani ndipo alipovamiwa na demu huyo wa mtu aliyekuwa amevaa nusu utupu na kuanza kucheza naye kwa staili mbalimbali tukio lililowafanya watu kulipuka kwa shangwe huku mgeni rasmi, Mbunge wa Kilosa, Mustafa Mkulo naye akiwa hana mbavu.
.
..Akazidi kujiachia na Tundaman.
Wakati Tundaman akiendelea kucheza na demu huyo, ghafla watu wote walishangaa kumuona demu huyo akimsukuma msanii huyo na kumwangusha chini kama gunia.
...Burudani zilipokolea akamdondosha chini Tundaman.
Aidha, demu huyo aliendelea kuwashangaza watu baada ya kumwangukia msanii huyo juu, ndipo wengine wakashtuka na kwenda kumsaidia Tundaman huku baadhi wakiendelea kucheka.
...Wakizidi kujiachia huku wakiwa chini.
Mabaunsa na madansa wa msanii huyo ndiyo walikwenda kumpa msaada kwa kumwinua huku demu huyo naye akishika ustaarabu wa kurudi sehemu aliyokuwa ameketi awali.
...Akishuka kutoka jukwaani.
Baada ya mrembo huyo kurudi sehemu yake, alikutana na kimbembe kwa kupewa kichapo kutoka kwa mtu wake ambaye alikuwa ametinga naye katika shoo hiyo.
Posted by Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment