Emmanuel Mgaya ‘Masanja’.
Mbali na muziki huo wa Injili kulipamba tamasha hilo, kutakuwa na mechi za mpira wa miguu kati ya wabunge wa Simba na wa Yanga huku Wasanii wa Bongo Fleva wakicheza na Bongo Movie
WANAMUZIKI wa muziki wa Injili Tanzania na Kenya wanatarajia kufanya tamasha kubwa la muziki wa Injili Afrika Mashariki Julai 7, mwaka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mratibu, Hudson Kamoga amesema tamasha hilo lenye lengo la kuchangia Mfuko wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), mwaka huu litakuwa na msisimko zaidi kwani limevuka mipaka ya Tanzania na kuwashirikisha wakali wanaotamba kwenye muziki huo nchini Kenya.
“Lengo ni kuiombea nchi yetu kupitia muziki wa Injili, waimbaji wa Kenya…
Mratibu, Hudson Kamoga amesema tamasha hilo lenye lengo la kuchangia Mfuko wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), mwaka huu litakuwa na msisimko zaidi kwani limevuka mipaka ya Tanzania na kuwashirikisha wakali wanaotamba kwenye muziki huo nchini Kenya.
“Lengo ni kuiombea nchi yetu kupitia muziki wa Injili, waimbaji wa Kenya watakutana na Watanzania na gospo ya ukweli itapigwa mfululizo,” alisema Kamoga.
TIMU YA KENYA
Kamoga amesema watakuwepo waimbaji wanaotamba nchini Kenya; Anastazia Mukabwa, Solomoni Mukubwa, Sara K na 24 Elders.
“Kila mtu anatambua nyimbo nzuri za Anastazia ikiwemo Kiatu Kivue, Solomoni Mukubwa anayetamba na wimbo wa Mfalme wa Amani na Sara K anayetamba na Liseme basi siku hiyo zitasikika live katika muziki mkubwa,” alisema.
TIMU YA TANZANIA
Kwa upande wa waimbaji wa nyumbani, Kamoga amesema wanamuziki wakali wanaotamba kama Upendo Nkone, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, Edson Masabwite, Ambwene Mwasongwe, Glorious Worship Team, Enock Jackson na Kundi la The Voice watakuwepo kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji na wote watakaofika uwanjani watapata kubarikiwa.
“Watakaofika siku hiyo watapata kuzisikia Usifurahi Juu Yangu wa Upendo, Tulipotoka ni Mbali wa Martha, Fanya Njia wa Mbasha na nyingine nyingi.
Edson Masabwite.
“Kama hiyo haitoshi watu watabarikiwa na
mwimbaji Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ anayetamba na wimbo wa Hakuna Jipya
bila kuwasahau Masabwite, Mwasongwe na Kundi la The Voice ambao wote
wataimba nyimbo nzuri za kumsifu Mungu,” alisema Kamoga.
Kamoga amewaomba Watanzania wanaoipenda nchi yao wajitokeze kwa wingi kumtukuza Mungu kwani sehemu ya mapato itakayopatikana kwenye tamasha hilo, itapelekwa kwenye mfuko wa elimu ambao utasaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike katika sekondari mbalimbali nchini.

0 comments:
Post a Comment