Kutokana na tukio la kinyama lililotokea Arusha, sitaweza kusoma
hotuba ya Bajeti Kivuli Bungeni. Wabunge wote wa CHADEMA tunaenda Arusha
kuomboleza, kutafakari na kuwapa moyo Watanzania wenzetu. Kufuatia
matokeo ya mchezo wa leo dhidi ya Ivory Coast, nimeona niwamegee kile
ningesema kuhusu Michezo.
Mheshimiwa Spika, maendeleo mazuri ya michezo katika taifa lolote, ni utambulisho mzuri wa taifa hilo katika mataifa mengine kutokana na ushirikiano wa kimichezo na mataifa hayo. Pamoja na mambo mengine, michezo katika nchi yetu inaweza kutumika kutengeneza fursa za kiuchumi kwa kuitangaza nchi yetu duniani katika sekta za utalii na uwekezaji. Ukiacha…
Kutokana na tukio la kinyama lililotokea Arusha, sitaweza kusoma hotuba ya Bajeti Kivuli Bungeni. Wabunge wote wa CHADEMA tunaenda Arusha kuomboleza, kutafakari na kuwapa moyo Watanzania wenzetu. Kufuatia matokeo ya mchezo wa leo dhidi ya Ivory Coast, nimeona niwamegee kile ningesema kuhusu Michezo. Soma natafakari...
MAENDELEO YA MICHEZO
Mheshimiwa Spika, maendeleo mazuri ya michezo katika taifa lolote, ni utambulisho mzuri wa taifa hilo katika mataifa mengine kutokana na ushirikiano wa kimichezo na mataifa hayo. Pamoja na mambo mengine, michezo katika nchi yetu inaweza kutumika kutengeneza fursa za kiuchumi kwa kuitangaza nchi yetu duniani katika sekta za utalii na uwekezaji. Ukiacha mbali suala la manufaa ya kiuchumi yanayoweza kupatikana kupitia michezo, michezo pia inawajengea vijana wetu afya na hivyo kuwa na taifa la watu wakakamavu. Kwa upande mwingine, michezo pia ni ajira. Inasikitisha kwamba katika hotuba nzima ya Waziri wa Fedha, hapakuwa na mpango wowote wa kukuza michezo hapa nchini bila hata kujali kwamba timu yetu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ipo katika nafasi nzuri sana hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote katika kuweza kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwakani.
Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika barua yake ya tarehe 5/4/2013 iliomba Kamati ya Bajeti kuangalia namna ya kusaidia kupata fedha za kujenga michezo na hasa kusaidia Taifa Stars katika juhudi zake za kuelekea kufuzu kwenye michuano ya kombe la Dunia huko Brazil. Hata hivyo Wizara ya Fedha haikutoa hata senti tano kwa ajili hiyo. Kamwe hatuwezi kufanikiwa kwenye michezo bila kuwekeza na kutegemea juhudi za dharura za kamati za kusaidia ushindi. Tukitaka tung’ae kwenye michezo ni lazima tuwekeze sana na kuwekeza ni gharama, gharama ambayo thamani yake ni kubwa sana kwa nchi.
Mheshimiwa Spika, licha ya michezo kuliingizia taifa mapato kupitia asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayotokana na viingilio katika michezo mbalimbali, hakuna uwekezaji wowote wa maana uliofanyika kwenye michezo jambo ambalo ni hatari kwa uhai na maendeleo ya michezo hapa nchini. Aidha hakuna mipango madhubuti ya muda mrefu kuhusu maendeleo ya michezo hapa nchini.
Kutowepo kwa mipango madhubuti na ya muda mrefu, kumeshababisha timu zetu kufanya vibaya katika mashindano mengi ya kimataifa na hivyo kulifanya taifa letu lionekane kuwa ni taifa dhaifu au kichwa cha mwendawazimu kama alivyopata kusema Rais Mstaafu was Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi. Kambi Rasmi ya Upinzani, inatoa angalizo kwa Serikali kwamba, kamwe hatuwezi kufanikiwa katika michezo kwa mipango ya kukurupuka. Aidha ni aibu kwa Serikali kukusanya kodi kutokana na michezo, halafu vijana wetu wanakosa fedha ya nauli kwenda nchi nyingine kwa mashindano ya michezo mpaka wafanye harambee ya kukusanya fedha kwa wahisani. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inapendekeza mambo yafuatayo yafanyike ili kunusuru tasnia ya michezo hapa nchini;
1. Timu yoyote itakayowakilisha taifa katika mashindano yoyote ya kimichezo igharamiwe na Serikali kwa asilimia 100.
2. Viwanja vyote vya Michezo hapa nchini viundiwe Wakala wa Serikali, Wakala wa maendeleo ya michezo (Sports Development Agency). Wakala huo uwe na majukumu ya kujenga viwanja vipya na kusimamia viwanja hivyo kwa niaba ya Serikali. Viwanja vyote vya michezo vilivyoporwa na CCM kama Lake Tanganyika – Kigoma, Ali Hasan Mwinyi - Tabora, Kirumba – Mwanza, Maji Maji – Songea nk virejeshwe Serikalini mara moja chini ya Wakala wa Viwanja vya Michezo. Wakala pia ujenge academies za michezo maeneo kama vile Mbeya, Tanga, Mtwara, Mwanza, Manyara na Dar es Salaam ili kukuza vipaji vya watoto na vijana.
3. Mashirika yote ya Umma, hasa mashirika makubwa yawe na timu za michezo. Ushauri uliotolewa na IMF na Benki ya Dunia dhidi ya Mashirika ya Umma kuwa na timu ulikuwa ushauri usio wa maana. Wenzetu Uganda kwa mfano, Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) wana timu katika ligi Kuu, ambayo ni moja ya timu mahiri katika ukanda huu wa bara la Afrika.
4. Serikali ianzishe Mfuko Maalum wa Michezo (Sports Fund). Pia, Serikali ianzishe Kodi ya Maendeleo ya Michezo (Sports Development Levy). Kodi hii ipatikane kama ifuatavyo: Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 18 iliyokuwa ikikatwa kwenye viingilio katika michezo mbalimbali iondolewe na badala yake kiasi hichohicho kiingizwe kwenye Mfuko wa Michezo (Sports Fund) utakaoanzishwa.
5. Matumizi ya Mfuko wa michezo yawe kama ifuatavyo:
i. Asilimia 50 ya fedha zitakazokusanywa zitumike kujenga miundombinu ya michezo (Sports Infrastructure) kupitia kwa Wakala wa Maendeleo ya Michezo na Academies.
ii. Asilimia 50 inayosalia itumike kuhudumia maandalizi ya timu za Taifa.WWW.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:
Post a Comment