Friday, February 21, 2014

LIGI KUU ENGLAND-WIKIENDI HII: UCHAMBUZI, TAARIFA, RATIBA YA MECHI ZOTE 10!


BPL2013LOGO
1545 Chelsea v Everton
1800 Arsenal v Sunderland
1800 Cardiff v Hull

1800 Man City v Stoke
1800 West Brom v Fulham
1800 West Ham v Southampton
2030 Crystal Palace v Man United
++++++++++++++++++++++++++++
CHELSEA v EVERTON
-Stamford Bridge
Nahodha wa Chelsea, John Terry, anatarajiwa kurudi baada kuzikosa Mechi 3 baada kujeruhiwa na hii itaimarisha ngome yao ambayo iliruhusu Bao 3 katika Mechi hizo alizokosa.
Hii ni Mechi ngumu na muhimu kwa Chelsea ambao ndio wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 1 mbele ya Arsenal.
Kwenye Mechi yao ya kwanza huko Goodison Park, Chelsea ilifungwa na Everton na Bao la ushindi kufungwa na Steven Naismith ambae amefunga Bao 4 katika Mechi 5 zilizopita.
CRYSTAL PALACE v MANCHESTER UNITED
-Selhurst Park
Baada ya kwenda huko Dubai kwa Kambi maalum ya Mazoezi ya kwenye Hali ya Joto, Mabingwa wa England, Manchester United, wamerudi na Jmamosi ndio watafunga dimba kwa Mechi za Ligi Kuu England kwa kucheza Ugenini huko Selhurst Park na Crystal Palace ambayo sasa imebadilika baada kupata Meneja mpya mzoefu, Tony Pulis.
Huku wakiichungulia Mechi yao ya Ugenini huko Ugiriki hapo Jumanne watakapocheza na Olympiacos kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Man United wanatarajiwa kidogo kubadili Kikosi chao.
Palace wao Januari waliimarika kwa kuongeza Wachezaji wapya na miongoni mwao ni Tom Ince, Mtoto wa Paul Ince, aliewahi kuichezea Man United.
ARSENAL v SUNDERLAND
-Emirates Stadium
Ni Mechi muhimu kwa Arsenal hasa baada ya Juzi kupigwa 2-0 Uwanjani kwao Emirates na Bayern Munich katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na hasa kwa vile wanakabiliwa na Mechi ngumu mfululizo zinazofuata dhidi ya Tottenham, Chelsea na Man City.
Lakini Arsenal wanakutana na Timu iliyofufuliwa upya chini ya Meneja Gus Poyet ambayo imefungwa Mechi 2 tu za Ligi katika 10 walizocheza mwisho.
CARDIFF CITY v HULL CITY
-Cardiff City Stadium
Cardiff City, chini ya Meneja mpya Ole Gunnar Solskjær, wana tatizo kubwa la ufungaji Magoli na kwenye Mechi hii watamkosa Kiungo wao muhimu kutoka Chile, Gary Medel, ambae ameumia.
Hull City wamejiimarisha kwa kuongeza Mastraika Nikica Jelavic na Shane Long lakini kazi yao kubwa ni kumpita Kipa mahiri wa Cardiff, David Marshall, anaetamba kuwa, pengine, ndie Kipa bora kwenye Ligi.
MANCHESTER CITY v STOKE CITY
-Etihad Stadium, 3pm
Baada kumshuhudia Lionel Messi, Neymar na Barcelona Juzi katiwiki walipopigwa 2-0 kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Jumamosi Etihad itamkaribisha Peter Crouch na Stoke City yake.
Mwanzoni mwa Msimu Stoke ilitoka 0-0 na Man City lakini Mechi hii ni ngumu kwao kuambua chochote hasa toka kwa City yenye machungu na ambayo inawania Ubingwa.
WEST BROMWICH ALBION v FULHAM
-The Hawthorns, 3pm
Fulham inatinga Mechi hii ikiwa na Meneja mpya toka Germany, Felix Magath na pia huenda Mchezaji wao mpya, Kostas Mitroglou, akaanza Mechi yake ya kwanza.
Hivi karibuni, WBA ilitoka Sare na Liverpool na Chelsea lakini pia imevujisha Bao 9 katika Mechi zao 4 zilizopita.
WEST HAM UNITED v SOUTHAMPTON
-Upton Park, 3pm
Katika Mechi 3 zilizopita, West Ham, chini ya Bosi Sam Allardyce, imekuwa ikishinda 2-0 kila Mechi na Nahodha wao Kevin Nolan kutikisa nyavu kila wakati huku Kipa wao Adrian akiwa ni shujaa.
Southampton, chini ya Meneja Mauricio Pochettino, ni Timu ngumu na hili pambano litavutia sana kwa ushindani wake.
LIVERPOOL v SWANSEA CITY
-Anfield, 1.30pm
Baada kutoka Sare 0-0 na Napoli Alhamisi Usiku kwenye EUROPA LIGI, Swansea inaivaa Liverpool Uwanjani Anfield.
Liverpool wanatoka huko Emirates walikofungwa 2-1 na Arsenal na kutupwa nje ya FA CUP huku Difensi yao ikileta wasiwasi baada kupachikwa Bao 6 katika Mechi 4 zilizopita.
NEWCASTLE UNITED v ASTON VILLA
-St James’ Park, 1.30pm
Faraja kubwa kwa Newcastle ambao hawajafunga hata Bao moja katika Mechi zao 4 zilizopita ni kurejea kwa Mfungaji wao hatari, Loic Remy, ambae alikuwa amefungiwa Mechi 3.
Mechi hii pia itamshuhudia Christian Benteke, ambae baada Magoli kukauka, hivi karibuni ameanza tena kucheka na nyavu kila mara.
NORWICH CITY v TOTTENHAM HOTSPUR
-Carrow Road, 4pm
Tottenham, chini ya Meneja mpya Tim Sherwood na Straika wao, Emmanuel Adebayor, alieibuliwa upya na Meneja huyo, wamekuwa wakifanya vyema tangu Meneja huyo ashike hatamu lakini Alhamisi huko Ukraine walichapwa Bao 1-0 huko Ukraine na FC Dnipro katika Mechi ya EUROPA LIGI ambayo Adebayor hakucheza.
Norwich City, chini ya Meneja Chris Hughton, wako kwenye hali mbaya hasa kwenye kufunga Mabao ambapo Mwaka huu 2014 wamecheza Mechi 9 na kufunga Bao 4 tu.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 23
1630 Liverpool v Swansea
1630 Newcastle v Aston Villa
1900 Norwich v Tottenham
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Chelsea
26
17
6
3
48
21
27
57
2
Arsenal
26
17
5
4
48
26
22
56
3
Man City
25
17
3
5
68
27
41
54
4
Liverpool
26
16
5
5
66
32
34
53
5
Tottenham
26
15
5
6
36
32
4
50
6
Everton
25
12
9
4
37
26
11
45
7
Man United
26
12
6
8
41
31
10
42
8
Southampton
26
10
9
7
37
29
8
39
9
Newcastle
26
11
4
11
32
38
-6
37
10
Swansea City
26
7
7
12
33
36
-3
28
11
West Ham
26
7
7
12
28
33
-5
28
12
Aston Villa
26
7
7
12
27
36
-9
28
13
Hull
26
7
6
13
25
31
-6
27
14
Stoke
26
6
9
11
27
41
-14
27
15
Crystal Palace
25
8
2
15
18
34
-16
26
16
Norwich
26
6
7
13
19
39
-20
25
17
West Brom
26
4
12
10
30
38
-8
24
18
Sunderland
25
6
6
13
25
38
-13
24
19
Cardiff
26
5
7
14
19
44
-25
22
20
Fulham
26
6
2
18
26
58
-32
20


0 comments:

Post a Comment