Marehemu Rodney Ndunguru (1985 - 2013) enzi za uhai wake.
Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea katika makaburi ya Mjimwema.
Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea katika makaburi ya Mjimwema.
Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi.
Mama wa marehemu Rodney Ndunguru baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la mwanaye.
SIMANZI,
Vilio, majonzi vimetawala wakati wa mazishi ya Askari wa Jeshi la
Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere
mkoani Morogoro ambapo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari
wa Jeshi la Wananchi ambao walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana
kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.
Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na
Paroko wa Kanisa Katoriki Jimbo Kuu la Songea Parokia ya Mjimwema,
Padre Noel Due ambaye wakati akiendesha ibada ya mazishi aliwaonya
Watanzania kutochezea amani na kwamba utulivu walionao Watanzania
unahitajika kulindwa kwa namna ya aina yeyote na si vinginevyo.Padre Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu tulionao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa Watanzania hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba huu.
Aidha Padri Due alimfagilia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa Jeshi la Polisi lihakikishe kuwa linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote badala ya kuibeza kwa kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya dola wakizani kuwa serikali haipo.
Kwa upande wake Kaimu wa Brigedi ya Kanda ya Kusini Kanari George Msongole alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney ilipokelewa muda mfupi baada ya kifo chake na kuwa Jeshi la Wananachi linaungana na familia ya marehemu katika majonzi na msiba mzito.
Kwa upande wake msemaji wa familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amesema kuwa familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao, na ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia ili waweze kujengewa nyumba ambayo itawasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.
Alisema kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na takribani miaka saba kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha pengo kubwa katika familia kwani katika uhai wake ilikuwa faraja kwa ndugu na jamaa.
Rodney Ndunguru alizikwa saa 10: 45 jioni kwenye makaburi ya Mjimwema ambako mamia ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma walihudhuria akiwemo mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu ambaye ni Katibu Tawala ya Wilaya ya Songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao
Posted by Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment