Cha msingi ni kufuata tu kanuni, kwani kwa
kufanya hivyo unaweza kwa kiasi kikubwa kuepukana na mambo mengi
yanayoweza kuhatarisha usalama wa kompyuta yako kama vile athari za
virusi.Ingawa mara nyingi husemwa kuwa hakuna usalama wa
asilimia mia moja kwenye ulimwengu wa teknolojia ya kompyuta, ila kinga
ni bora kuliko tiba.
Umewahi kujiuliza kwa nini watu wengi wanatumia kiasi kikubwa cha fedha kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ya makazi?
Ndivyo ilivyo, tembelea hata katika makazi ya watu
wa kawaida, madirisha yamejaa nondo, nyumba zimezungukwa na kuta
ndefundefu. Wengine wamefikia hatua ya kufuga mbwa kwa ajili ya
kuwalinda.
Nimeanza kwa kutoa mifano hii kuonyesha umuhimu wa
kuzilinda kompyuta zetu. Ingawa mara nyingi husikika ikisemwa kuwa
hakuna usalama wa asilimia mia moja kwenye ulimwengu wa teknolojia ya
kompyuta, ila kinga ni bora kuliko tiba.
Cha msingi ni kufuata tu kanuni, kwani kwa kufanya
hivyo unaweza kwa kiasi kikubwa kuepukana na mambo mengi yanayoweza
kuhatarisha usalama wa kompyuta yako kama vile athari za virusi.
Makala haya yanataja baadhi ya kanuni za msingi unazopaswa kufuata ili kutunza usalama wa kompyuta yako.
Tumia programu unazozihitaji
Watumiaji wengi wa kompyuta tumekuwa waathirika wa
matatizo ya kompyuta zetu ama kwa kujua au kwa kutokujua. Kwanza
ieleweke kuwa kompyuta nyingi zimekuwa zikiathiriwa kiusalama kwa
makosa yaliyomo kwenye kompyuta husika.
Hizi ni zile kompyuta zenye programu ambazo
hazijaandikwa kiusahihi. Tuchukue mfano wa nyumba inayovuja, kwa kuwa
tu paa lake halikuezekwa ipasavyo. Au ukuta wa nyumba unavyoweza
kuanguka, kwa kuwa haukutengenezwa kwa kufuata taratibu za ujenzi.
Kama kompyuta yako ina programu ambayo
haikuandikwa kwa usahihi, matatizo mengi hutokea yanayoweza kuhatarisha
kifaa hicho. Programu hizi sio tu zitahitilafiana na mtambo endeshi (OS)
wa kompyuta yako, pia zinaweza kutoa mianya kwa wavamizi kuingia
kwenye kompyuta yako kupitia kwenye mianya iliyopo kwenye programu
hizi.
Cha kufanya: Mosi, ondoa programu usizotumia.
Tuache tabia ya kuweka programu nyingi katika kompyuta zetu ambazo kwa
hali ilivyo hatuzitumii kabisa. Kwa kawaida programu hujaza nafasi,
kuweka uchafu na hatimaye kuiweka kompyuta matatani.
Kumbuka unapoweka (install) baadhi ya programu
katika kompyuta yako, nazo huweka programu nyingine zinazoambatana nazo
bila ya wewe kujua. Hatimaye unajikuta umelundika lundo la programu.Posted byhttp://thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment