Sunday, September 15, 2013

LIGI ULAYA: BALE AFUNGUA UKURASA MPYA

BALE_IN_REAL

JANA, Real Madrid walimwanua rasmi Mchezaji Ghali Duniani, Gareth Bale, afanya mambo yake bale ambae alifunga Bao moja na Supastaa mwenzake Cristiano Ronaldo kufunga Bao jingine wakati Real wakiambulia Sare na huko Italy, kwenye mtanange wa Derby D’Italy, Inter Milan na Juventus zilitoka Sare.


>>DERBY D’ITALIA: INTER 1 JUVE 1
>>BUNDESLIGA: DORTMUND YAFUMUA 6!!
SERIE A: INTER 1 JUVENTUS 1
Uwanjani San Siro hapo Jana, Inter Milan na Juventus zilitoka Sare ya Bao 1-1 katika Mechi spesheli iliyobatizwa Derby D’Italy.
Inter ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 73 kwa Bao la Mauro Icardi na Juve kurudisha Dakika 2 baadae kwa Bao la Arturo Vidal.
BUNDESLIGA: DORTMUND 6 HAMBURG 2
Borussia Dortmund Jana ndani ya Signal-Iduna-Park walilipa kisasi cha Msimu uliopita kufungwa 4-1 na Hamburg na kuibamiza Hamburg Bao 6-2 katika Mechi ya Bundesliga.
Bao za Borussia Dortmund zilifungwa na Robert Lewandowski na Pierre-Emerick Aubameyang, Bao 2 kila mmoja, Marco Reus na Mkhitaryan, Bao 1 kila mmoja.
Bao za Hamburg zilifungwa na Zhi Gin Lam na Heiko Westermann
Mapema hiyo Jana, Mabingwa Watetezi Bayern Munich waliichapa Hannover Bao 2-0 na Bao zao kufungwa na Franck Ribey na Mandzukic.
Kwenye Bundesliga, Borussia Dortmund wanabaki kileleni.
LA LIGA: BARCA 3 SEVILLA 2, VALENCIA 2 REAL 2
Mabingwa Watetezi Barcelona waliichapa Sevilla Bao 3-2 hapo Jana kwenye Mechi ya La Liga na Bao zao kufungwa na Alves, Lionel Messi na Sanchez wakati Bao za Sevilla zilifungwa na Rakitic na Coke.
Nao Real Madrid, wakimchezesha Mchezaji Ghali Duniani, Gareth Bale, kwa mara ya kwanza, walitoka Sare ya Bao 2-2 walipocheza Ugenini na Villareal huku Bale akisawazisha Bao baada ya Cani kuipa Bao la kwanza Villareal.
Cristiano Ronaldo akaifungia Real Bao la Pili lakini Villareal wakasawazisha kwa Bao la Dos Santos.

0 comments:

Post a Comment