Monday, January 27, 2014

Wachezaji walevi Yanga kukiona


Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu amekemea tabia ya baadhi wa wachezaji wa timu yake kuendeleza unywaji pombe na uvutaji wa sigala.
Na kwa sababu hiyo, ameamua kukutana na wachezaji ili kuwaeleza hatari ya tabia hizo.
“Utovu wa nidhamu unaanzia toka utotoni, hapa kwetu wachezaji wengi wanaocheza soka ni wale walioishia darasa la saba, wanashindwa kujitambua,” alisema Benno.
Aliongeza: “Kuna haja gani ya mtu kama mimi namfuatilia mchezaji asinywe pombe, wakati anajua fika kwa kufanya hivyo ni kuharibu kiwango chake.”
Benno alisema tabia ya baadhi ya wachezaji kupenda kucheza mechi za ‘ndondo’ nayo ni mzigo mkubwa kwa klabu, kwani akiumia jukumu la matibabu hubebwa na klabu iliyomsajili.
Kauli ya Njovu imekuja kukiwa na taarifa kuwa tayari uongozi wa Yanga unatarajia kuwakata mshahara wachezaji, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Haruna Niyonzima, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, David Luhende, Simon Msuva na Athuman Idd ‘Chuji’ ambaye anapewa nusu mshahara baada ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.
Habari za uhakika ambazo Mwananchi ilizipata kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo zilisema kuwa licha ya uongozi kumtaka Chuji kujirekebisha, amekuwa akikaidi.
Hata hivyo Njovu alipoulizwa suala la mchezaji huyo, alisema:  “Chuji yupo anatumikia adhabu aliyopewa mpaka hapo uongozi utakapotoa taarifa zaidi.”poste by http://thesuperonenews.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment