Monday, January 27, 2014

Faida,// hasara usajili ghali wa Man U


Wiki iliyopita, kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson alisema timu sita ikiwamo Manchester United ndiyo zenye nafasi kubwa ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya England ingawa hakuitaja Liverpool.
Ferguson ambaye bado ni mkurugenzi katika klabu ya Manchester United alisema hivi sasa klabu ya Manchester
City ndiyo inayoonekana kama ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, lakini anaona itashindwa kufanya vizuri katika mechi za mwishoni mwa ligi.
“Ligi ilivyo bado siyo nyepesi kutwaa ubingwa, unaweza kusema hivi sasa Manchester City wanacheza vizuri, lakini timu ambayo inaongoza msimamo wa ligi hivi sasa ndiyo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa,” alisema Ferguson.
Alisema, “Arsenal ndiyo ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, lakini nashangaa watu wengi hawaipi nafasi, lakini wamesahau tupo katika mzunguko wa pili wa ligi na bado wanakaa kileleni.”
Ferguson alisema, “Pia zipo timu kama Chelsea, Everton na Tottenham ambazo zinafanya vizuri na zina nafasi ya kutwaa ubingwa, Manchester United kila msimu huwa inafanya vizuri zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi kwa hiyo ninatarajia itafanya vizuri pia kwani ina falsafa na historia nzuri.”
Hata hivyo Manchester United ambayo hivi sasa ipo chini ya kocha mpya David Moyes imekuwa ikisuasua katika Ligi Kuu ya England na hivi sasa inashika nafasi ya saba.
Pia Manchester United imetolewa katika mashindano ya kombe la FA na kombe la ligi (Capital One) ingawa bado wapo katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kutokana na Manchester United kushindwa kupata matokeo mazuri, hivi sasa zipo taarifa mbalimbali kwamba kocha Moyes anaweza kutimuliwa. Hata hivyo kocha Alex Ferguson amemtetea kocha huyo na kusema hatakiwi kutimuliwa ila anahitaji kupewa muda na kufanya usajili.
Tayari kocha Moyes ameanza kusajili, ambapo Manchester United imekubali kumwaga fedha na kumsajili kiungo mshambuliaji Juan Mata kutoka Chelsea ambaye gharama yake ni pauni 37milioni, ambazo ni fedha nyingi.
Wafuatao ni baadhi ya wachezaji 10 ambao United ilitumia fedha nyingi kuwasajili, ambapo gazeti la Sportstmail linaelezea namna wengine walivyokuwa msaada na wengine kushindwa kuwa msaada kwa klabu hiyo.
1.Dimitar Berbatov Pauni 30.75mil (Tottenham)
Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson hakuwa wazi namna alivyoweza kumnasa mshambuliaji huyo wa Bulgaria, japokuwa rekodi yake ya mabao 56 katika mechi 149 ilikuwa ya kuvutia. Lakini pamoja na ukubwa wa umbo lake, mchango wake haukuwa kama kocha Ferguson aivyotaka, kwa hiyo hakuwa msaada kwa klabu hiyo.posted by thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment