Monday, January 27, 2014

KWA MARA NYINGINE TENA WANAKUTANA : MAN CITY v CHELSEA,,, ARSENAL v LIVERPOOL!! NAN MKALI!!!!


FA_CUP_LOGO_NEW
DROO ya Raund ya 5 ya FA CUP imefanyika hii Leo na kuibua Mechi za Mvuto mkubwa kwa kupambanisha Vigogo ambapo Manchester City itaivaa Chelsea na Arsenal kukutana na Liverpool.

Mechi zingine zitakazohusisha Timu za Ligi Kuu England ni zile kati ya Sunderland v Southampton na Everton v Swansea.
Mechi hizi zitachezwa Wikiendi ya Febbruari 15 na 16 na Washindi kutinga Robo Fainali.
Droo hiyo ilifanyika huko Wembley Stadium Jijini London na kuendeshwa na Andros Townsend, Mchezaji Chipukizi wa Tottenham, pamoja na Baba yake Mzazi, Troy, ambae ni Mwanaharakati maarufu kwenye Soka.
FA CUP
RAUNDI YA 5
[Mechi kuchezwa Februari 15 & 16]
DROO KAMILI
Manchester City v Chelsea
Sheffield United AU Fulham v Nottingham Forest AUr Preston NE
Arsenal v Liverpool
Brighton v Hull
Cardiff City v Wigan
Sheffield Wednesday v Charlton
Sunderland v Southampton
Everton v Swansea
+++++++++++++++++++++++++++++
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
TAREHE ZA RAUNDI:
-RAUNDI YA 3: Jumamosi Januari 4 [KLABU ZA LIGI KUU ENGLAND HUANZA]
-RAUNDI YA 4: Jumamosi Januari 25
-RAUNDI YA 5: Jumamosi Februari 15
-RAUNDI YA 6: Jumamosi Machi 8
-NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
-FAINALI: Jumamosi Mei 17   Posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment