Friday, January 17, 2014

MOYES WASIWASI MWIGI KWA MASTAA WAKEI!!

MOYES-OLD_TRAFFORD_TOUCHLINE
MENEJA wa Manchester United David Moyes amethibitisha kuwa Mastraika wake mahiri Wayne Rooney na Robin van Persie wataikosa Mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu England huko Stamford Bridge dhidi ya Chelsea.

Mastaa wote hao wawili, licha ya kuanza tena Mazoezi wakitokea kwenye maumivu ya Nyonga kwa Rooney na Paja kwa Van Persie, bado hawajawa fiti kwa ajili ya Mechi.
Akiongea na Wanahabari hii leo, Moyes alisema: “Wayne hayuko tayari kwa Chelsea. Ameanza tena Mazoezi ya kukimbia na kuimarisha Nyonga yake.”
Kuhusu Van Persie, Moyes alisema: “Nategemea Robin kuanza Mazoezi Wiki ijayo. Tunataka arudi haraka. Ni Mchezaji muhimu kwetu. Tumewakosa sana Wachezaji hawa wawili lakini wanakaribia kuwa fiti.”
Pia Moyes alithibitisha kutolewa kwa Mkopo kwa Kiungo kutoka Brazil, Anderson, ambae ameenda Klabu ya Italy inayochezaANDERSONSerie A Fiorentina.
Amesema: “Hapa hakuwa akicheza Mechi nyingi. Hii ni nafasi nzuri kwake kwenye Klabu nzuri na Ligi nzuri.”
Vile vile, Moyes amepuuza uvumi wa sababu za yeye kuonekana kwenye Mechi za Juventus na Paris St Germain na amedai: “Mimi napenda kutazama Soka Duniani kote. Si Siku zote nakuwepo kwenye Mechi ili kusaini Wachezaji. Wakati mwingine ni kujielimisha tu. Nimetembea sehemu nyingi hivi karibuni.”
Kuhusu uhusiano wake na Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea, Moyes amedokeza uko poa licha ya Vyombo vya Habari kutaka kuonyesha ipo bifu hasa baada ya Mourinho kutaka kumchukua Wayne Rooney mwanzoni mwa Msimu.
Moyes ameeleza: “Hatuwezi kumuuza Wayne Rooney hivyo uhusiano wangu na Jose uko safi. Namheshimu kwa mafanikio yake na jinsi anavyosimamia Klabu zake. Ni mmoja wa Mameneja Bora wa kisasa na pengine atakuwa mmoja wa Bora zaidi kwenye historia. ”
MECHI ZA MAN UNITED ZINAZOFUATA:
Jumapili Januari 19
Chelsea v Man United [Ligi Kuu England]
Jumatano Januari 22
Man United v Sunderland [Capital One Cup-Nusu Fainali Marudiano]
Jumanne Januari 28
Man United v Cardiff [Ligi Kuu England]  Posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment