Mbwa ni mnyama wa kufugwa mwenye manufaa chekwa.
Anaisaidia jamii kwa mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi, kazi za kiusalama
na hata utunzaji wa mazingira.
Kwa sababu anaishi kwa ukaribu kabisa na wanajamii anahitaji kutunzwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanapata chanjo.
Hali katika Mkoa wa Dodoma, imekuwa kinyume kwa
sababu kumekuwa na idadi kubwa ya mbwa wanaozurura mitaani jambo ambalo
linahatarisha maisha ya wakazi.
Uchunguzi uliofanywa katika maeneo mbalimbali
ulibaini kuwa kuna idadi kubwa ya mbwa wanaozurura ovyo kwenye maeneo ya
Area A, Swaswa, Area D na hata katikati ya mji.
Aghalabu siku haiwezi kwisha bila kuona mbwa
akikatisha katika mitaa ya katikati ya mji, wakati wa mchana bila kuwa
chini ya uangalizi.
Ofisa Mfuatiliaji wa Mgonjwa yanayotokana na chanjo mkoni hapa, Paul Mgeni, anasema tatizo la watu kung’atwa na mbwa ni kubwa.
“Si chini ya watu 10 ambao wamekuwa wakiripoti
katika hospitali yetu (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma) kuwa
wameumwa na mbwa na hasa hasa wanaoathirika ni watoto wadogo,” anasema.
Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha kati
ya Januari na Oktoba mwaka jana, jumla ya watoto 278 walio chini ya
umri wa miaka mitano waling’atwa na mbwa mkoani hapa.
Kati ya hao watoto 165 walikuwa ni wa kiume wakati
watoto 113 walikuwa ni wa kike. Kwa mujibu wa takwimu hizo watu zaidi
ya umri wa miaka mitano waliong’atwa na mbwa katika kipindi hicho,
walikuwa ni 1580 ambapo kati ya hao wanaume walikuwa 931 wakati wanawake
walikuwa 649.
Mwaka juzi, watoto chini ya miaka mitano walikuwa ni 326 na waliojuu ya miaka mitano walikuwa ni 877.
Mageni anasema watu 16 walipoteza maisha mkoani hapa kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Hata hivyo anasema wengi wa watu wanaokuja kupata matibabu hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua chanjo.posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment